Baadhi
ya wananchi na viongozi wanapaswa
kuelewa kwamba tume huru ,ambayo
viongozi wake watapatikana KWA bila kuteuliwana Rais itatokana baada maoni yaliyopo katika Katiba Pendekezwa
kupitishwa kwenye kura ya maoni.
Hayo yamesemwa na Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi(NEC), Damian Lubuva, jana
wakati alipotembelea kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba)
yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo iliotolewa na Jaji Lubuva kwenye Banda la NEC lililopo ukumbi wa Jakaya Kikwete na banda la Mahakama ya
Tanzania wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari.
Alisema
dhana ya tume huru nadhani baadhi ya watu
wengi hawajaielewa, hivyo maana yake ni
uwezo wa kujiendesha na kujisimamia bila
kuingiliwa.
Aidha Jaji Lubuva amesema kwamba NEC haijawahi
kuingiliwa kiutendaji kama inavyodaiwa
na baadhi watu wanaofikiria hivyo, kwa kuwa ni tume huru inafanya kazi zake za uendeshaji
na kujisimamia yenyewe.
“Sisi tuliotoa
maoni katika Tume ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba kuwa Mwenyekiti wa NEC, Makamu wake na
makamshina wasiteuliwe na Rais ili kuepusha fikira kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi sio huru,” alisema Jaji Mstaafu Lubuva.
Aliongeza kwamba
NEC ni tume huru, kwani yeye alikuwa ni
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara(SADCC), hivyo nchi hizo ziliisifia
Tanzania kutokana na uendeshaji wake wa
shughuli za uchaguzi, huku akisema nabii huwa hasifiwi nyumbani.
“Nimekua na
uhusiano mzuri na SADCC tulikuwa Angola
na Msumbiji kiutendaji wamevutiwa na sisi,” alisisitiza.
Alisema
Umoja wa nchi za Ulaya pia uliridhika
uchaguzi ulienda vizuri pamoja na maandalizi yake. Hivyo uchaguzi ulienda
vizuri matokeo yaliyotolewa ndio wananchi waliamua.
Jaji Lubuva
alifafanua kwamba hivi sasa NEC wako katika maandalizi ya kuhakikisha kwamba
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 utakafanyika
kwa utaratibu mpya, kwa kuwa wameanza maandalizi ili shughuli za
uandikishaji ziwe endelevu. Alisema kwa
sasa wameaanza kuandikisha watu waliotimiza umri wa miaka 18.
Akizungumzia kuhusu kura ya maoni alisema
itafanyika kabla ya mwaka 2020, hivyo utaratibu mpya utaondosha dhana hiyo.
Jaji Lubuva alisema hivi sasa wanaweka msingi ili kuuwezesha uchaguzi ujao kufanyika kwa
ubora na ufanisi, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.
Jaji Mstaafu,Mhe. Damian Lubuva (aliyenyoosha kidole) akitembelea Maonyesho 40 ya Biashara ya Kimataifa yajulikanayo kwa jina la sabasaba katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dares Salaam . |
Waziri
wa Katiba na Sheria,Mhe, Dkt. Harrison Mwakyembe, kizungumza na baadhi
ya waandishi wa habari wakati akitembelea maonyesho ya sabasaba. |
Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe, Dkt. Harrison Mwakyembe, kizungumza na baadhi ya waandishi wa habari wakati akitembelea maonyesho ya sabasaba. |
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mheshimiwa Katarina Revokati akifungua kikao kazi cha kuandaa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania kati ya Menejimenti ya Mahakama na Wadau wanaofanya kazi pamoja na Mahakama. Katika ufunguzi huo Mheshimiwa Revokati aliwashukuru wadau hao kwa kutoa mchango wao wa mawazo uliouboresha Mpango Mkakati huo ambapo alisema michango hiyo imeupa sura ya Utekelezaji.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina Revokati (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha kuandaa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Mahakama ya Tanzania pamoja na wadau wanaofanya kazi na Mahakama wakifuatilia jambo wakati wa kuandaa Mpango Mkakati wa Mahakama leo jijini Dar es salaam. Baadhi ya wadau hao ni pamoja na Tanganyika Law Society, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Takukuru,na Wakala ya Serikali Mtandao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni