Jaji Mstaafu Damian Lubuva akiangalia kikapu cha asili ya Kitanzania wakati akitembelea Maonyesho ya 40 Biashara ya Kimataifa yajulikanayo kwa jina la
sabasaba katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dares Salaam .
Jaji Mstaafu Damian,Mhe. Lubuva amesema Tanzania imepiga hatua katika kuboresha
bidhaa zinazozalishwa hapa nchini, hivyo
inaweza kushindana na bidhaa za nje.
Hayo
yamesemwa na Jaji Mstaafu, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC),Mhe. Lubuva, wakati alipotembelea katika Maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa (sabasaba) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. J.K.
Nyerere jijini Dar es Salaam kwenye Banda la NEC lililopo ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Jaji Lubuva
alisema hayo wakati akifanya mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari mara
baada ya kutembelea Banda la Jakaya Kiwete, Pride Tanzania, Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mahakama ya Tanzania,
na Jeshi la Kujenga Taifa.
“ Bei za
bidhaa zetu ni za gharama nafuu , sasa tujiendeleze kwa kuwa viwanda kama Serikali ya Awamu ya Tano
inavyosisitiza, tunaweza kushindana na
bidhaa za nje,alisema,”Mhe. Jaji Lubuva.
Akizungumzia
kuhusu ziara yake katika maonyesho hayo, alisema ametembelea ili aweze kujifunza baadhi ya
mambo muhimu.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni