Mkuu wa
Jeshi la Polisi la Malawi, Lexten Kachama, (aliyevaa suti) akiangalia Mpango
Mkakati ya Utendaji kazi wa mwaka 2015/2016 hadi 2019/2020.Kushoto Naibu Msajili
Mwandamizi Mahakama Kuu , Mhe. Eva Nkya kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwl.J.K.
Nyerere jijini Dar es Salaam , barabara ya Kilwa.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi la Malawi, Lexten Kachama ameipongeza nchi ya Tanzania kwa juhudi
zake za kupambana na mauaji ya albino (watu wenye ulemavu wa ngozi).
Aidha Mkuu
huyo amesema Tanzania imefurahishwa na uhusiano mzuri wa utendaji kazi kati ya Mahakama ya Tanzania na Jeshi la Polisi,ambao umerahisisha
usikilizaji wa kesi mbalimbali, zikiwemo za albino kwa wakati.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Mkuu huyo mara baada ya kutembelea banda la Mahakama ya Tanzania kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwl.J.K.
Nyerere jijini Dar es Salaam , barabara ya
Kilwa.
Aidha Kachama amesema ametembelea banda la Mahakama ya Tanzania, kwa sababu utendaji kazi wa Mahakama na Jeshi la Polisi ni wa Ushirikiano.
Aidha Kachama amesema ametembelea banda la Mahakama ya Tanzania, kwa sababu utendaji kazi wa Mahakama na Jeshi la Polisi ni wa Ushirikiano.
“Tanzania ni
nchi ambayo imefanya vizuri kutokana na jitihada zake za kupambana
vita dhidi ya mauaji ya albino. Nimeshuhudia kuhusu takwimu kesi za mauaji ya kesi mbalimbali, zikiwemo zinazohusu albino.
Hii
inaonyesha ni jinsi gani kati ya Mahakama na Jeshi la
Polisi walivyo na uhusiano mzuri
wa utendaji kazi,” alisema IGP Kachama,huku akisisitiza kwamba uhusiano huo unapaswa kuendelea kuendelezwa.
Mkuu huyo
aliongeza kwamba Tanzania ni nchi ya mfano wa kuigwa katika husiano huo, ingawa
zipo nchi nyingine zinafanya vizuri pia.
Alisema
viongozi wa nchi hizo mbili, Rais wa
Malawi, Arthur Peter Mutharika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Pombe Magufuli pia wanamahusiano mazuri. Hivyo uhusiano huo umewaweka
Wamalawi na Watanzania pamoja.
“Nimefurahi
kutembelea Tanzania, ni nyumbani, pia nimefurahishwa na maonyesho mazuri,
pia niwashukuru Watanzania
kwa ukarimu wao,” alisema IGP
huyo, huku akiwatakia waendelee kuishi kwa amani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni