Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mheshimiwa Katarina Revokati akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mahakama ya Tanzania unaoandaa Mpango Mkakati wa Mahakama hiyo leo katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mheshimiwa Mwanaisha Kwariko akizungumza kwenye Mkutano wa Mahakama ya Tanzania wa kuandaa Mpango Mkakati wa Mhimili huo leo mjini Dodoma
Wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa Mahakama ya Tanzania kuhusu Mpango Mkakati wakiwa tayari kuanza mkutano huo leo katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. wajumbe hao ni Mahakimu wafawidhi wa mikoa na wilaya, wasajili wa mahakama, watendaji wa Mahakama pamoja na wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania makao Makuu
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Frednand Wambali (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Mikoa na Wilaya nchini baada ya kufungua Mkutano kuhusu Mpango Mkakati leo katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Frednad Wambali(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wasajili wa Mahakama nchini baada ya kufungua Mkutano kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania leo katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Frednand Wambali (wa nne kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mahakama nchini mara baada ya kufungua Mkutano wa kuandaa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania leo mjini Dodoma
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Frednand Wambali (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania Makao Makuu mara baada ya kufungua Mkutano kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama hiyo leo mjini Dodoma
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Frednand Wambali akisaini kitabu cha wageni alipotembelea ofisi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma leo mkoani humo
WATUMISHI
WA MAHAKAMA WATAKIWA KUFUATA MAADILI
Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu Mheshimiwa Ferdinand Wambali amewataka watumishi wa Mahakama nchini kufanya
kazi kwa kufuata maadili na misingi ya haki ili wananchi waweze kujenga imani kwa
mhimili wa Mahakama pamoja na wadau wengine wa utoaji wa haki.
Akifungua Mkutano unaoandaa
Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania leo mjini Dodoma, Jaji Kiongozi alisema
iwapo watumishi wa mahakama watafanya kazi kwa bidii na kwa kufuata maadili na
misingi ya haki, mahakama itaaminika zaidi kwa wananchi.
Akizungumzia suala la
maadili kwa Majaji na Mahakimu wa mahakama zote nchini, Mheshimiwa Wambali
alisema maadili kwa watumishi hao hayaishii mahakamani peke yake bali yanaende
hata nje ya Mahakama hivyo aliwataka watumishi hao kuishi kwa kufuata maadili
mema mbele ya jamii inayowazunguka.
Alisema suala la imani ya
wananchi kwa Mahakama ya Tanzania ni moyo wa mhimili huo wa utaoji wa haki
nchini hivyo wakati wote chombo hicho kinapaswa kuwa na muonekano chanya.
Akizungumzia Mkutano kuhusu
Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, Mtendaji wa Mahakama ya Biashara, Willy
Machuma aliwaambia waandishi wa habari kuwa lengo la Mkutano huo uliojumuisha
pia wadau wa utoaji haki nchini ni kukaa pamoja na kupanga namna ya kuutekeleza
mpango Mkakati ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na mahakama
kuwa na muonekano chanya mbele ya wananchi.
Mkutano huo wa siku kumi
ulioandaliwa na Mahakama ya Tanzania unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 132
kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiwemo Mahakimu wafawidhi wa mikoa na wilaya,
wasajili wa Mahakama, watendaji wa Mahakama, na wadau wa utoaji wa haki nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni