Jumatatu, 10 Oktoba 2016

MAHAKAMA YA TANZANIA YASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA YANAYOFANYIKA KITAIFA MKOANI SIMIYU


Vijana wa Halaiki wakiandamana wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Wiki ya Vijana Kitaifa inayofanyika Mkoani Simiyu. Mahakama ya Tanzania nayo imeshiriki kwenye Wiki hiyo 
 
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakielimishwa juu ya utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea banda la Mahakama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jennister Mhagama akifungua rasmi Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa Mkoani Simiyu.


Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu Mheshimiwa John Francis Nkwabi akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania kwa Mwananchi aliyetembelea banda la Mahakama kwenye Maonesho ya Vijana ya Kitaifa yanayoendelea mkoani humo.  


Muonekano wa Banda la Maonesho la Mahakama ya Tanzania 

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu Mheshimiwa John Francis Nkwabi akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania kwa Wananchi waliotembelea banda la Mahakama kwenye Maonesho ya Vijana ya Kitaifa yanayoendelea mkoani humo.


Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakipata Elimu kwenye Banda la Mahakama katika Maonesho ya Wiki ya Vijana ya Kitaifa yanayoendelea mkoani humo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni