Jaji Mkuu wa Australia
ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akipokea zawadi ya picha
kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika halfla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba wa Mahakama
ya Rufani ya Tanzania. Mhe. Jaji Kourakis alimaliza ziara yake nchini mnamo tarehe 07.10.2016.
Waziri wa Katiba na
Sheria,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)akizungumza na Jaji Mkuu wa Australia
ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis(katikati) na (kulia) ni Msajili
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,Bi.
Katarina Revocati katika mkutano huo ulifanyika leo tarehe kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya
Katiba na Sheria uliopo jijini Dar es
Salaam.
Jaji Mkuu wa Australia
ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis akiangalia na kupata maelezo juu ya mfumo wa kielektroniki wa kusajili mashauri kutoka kwa Karani wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopo jijini Dar es Salaam Bw.
Abdallah Bugalo wakati alipoitembelea leo .
Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kulia) akizungumza kuhusu ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya mafunzo, sheria na shughuli za kimahakama baina ya nchi hizo mbili. (kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe. Mkutano huo ulifanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria uliopo jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni