Jaji Mkuu wa Australia, Mhe. Christopher
Kourakis (kulia) alipowasili katika Bandari Kuu ya Zanzibar kukutana na
Mwenyeji wake Jaji Mkuu- Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu kwa lengo la
kubadilishana uzoefu katika utendaji
kazi wa Mahakama.
1
Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.
Christopher Kourakis akisaini kitabu cha wageni pindi alipowasili Mahakama Kuu
Zanzibar, katika Ofisi ya Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Mhe. Omar Othman Makungu.
Mrajisi Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mhe.
George Joseph Kazi akisoma taarifa ya Mahakama hiyo mbele ya Jaji Mkuu wa
Australia Kusini pindi alipowasili katika Mahakama hiyo kwa lengo la
kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wa Mahakama.
Jaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Omar Othman
Makungu akiongea jambo alipofanya mazungumzo na mgeni wake, Jaji Mkuu wa
Australia Kusini alipowasili ofisini kwake, katika mazungumzo yao, Mhe. Jaji Mkuu huyo alisema kuwa Mahakama-Zanzibar ipo katika mchakato wa maboresho ikiwa ni pamoja na
kuwa maktaba ya kidijiti n.k
1 Jaji Mkuu wa Australia Kusini alipofanya
mazungumzo na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar alipotembelea katika
Mahakama hiyo.
1.
Jaji Mkuu- Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu
(kulia) akimpatia mgeni wake zawadi ya kitabu cha Sheria mbalimbali za
Zanzibar.
1
Jaji Mkuu wa Australia Kusini akikabidhi
zawadi kwa Jaji Mkuu wa Zanzibar
1
Mrajisi-Mahakama Kuu Zanzibar
akimpitisha Jaji Mkuu wa Australia Kusini katika ofisi mbalimbali za Mahakama
Kuu Zanzibar
Mhe. Mrajisi akimuonesha kitu Jaji Mkuu
wa Australia Kusini walipokuwa katika moja ya kumbi za Mahakama Kuu Zanzibar.
1 Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman
Makungu (katikati), Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe. Christopher Kourakis
(wa pili kushoto), Mhe. Sekiet Kihio, Jaji wa Mahakama Kuu-Tanzania wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji na Warajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar
Jaji Mkuu huyo pia alitembelea sehemu
mbalimbali za Kihistoria katika nchi hiyo ikiwa ni pamoja na Kanisa la
Mkunazini, Jumba la kumbukumbu ya historia ya Zanzibar, Jumba la Baraza la
Wawakilishi na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni