Na, Mary Gwera
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema leo (23.12.2016) amewaapisha
Majaji wanne wa Mahakama ya Rufani (T), Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) na Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo
iliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa ikiwa ni pamoja na Waziri
Mkuu, Jaji Mkuu, Waziri wa Utumishi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengineo,
Mhe. Rais alianza kumuapisha Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambaye kabla ya uteuzi wake, Mhe.Kaijage alikuwa ni
Jaji wa Mahakama ya Rufani (T).
Aidha; Mhe. Rais pia
amemuapisha Mhe. Harold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T) kuwa
Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma.
Hali Kadhalika Mhe.
Rais amewaapisha jumla ya Majaji wanne walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya
Rufani (T), ambao ni Mhe. Rehema Mkuye, Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Mhe. Dkt.
Gerald Ndika na Mhe. Jackobs Mwambegele.
Kabla ya uteuzi huo,
Mhe. Jaji Rehema Mkuye alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa
ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Mwangesi alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-
Divisheni ya Ardhi, Mhe. Ndika alikuwa Jaji-Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi,
na Mhe. Mwambegele alikuwa Jaji- Mahakama Kuu- Divisheni ya Biashara.
Akizungumza baada ya
uapisho huo, Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Rehema Mkuye amesema atafanya
kazi kwa ushirikiano pamoja na Majaji wengine wa Mahakama hiyo.
“Namshukuru Mhe. Rais
pamoja na Uongozi wa Mahakama kwa nafasi hii, nami ninahaidi kwa dhati
nitafanya kazi ya kuwatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na
wenzangu nitakaowakuta,” alisema Jaji Mkuye.
Hali kadhalika Majaji
wengine Wateule wamehaidi pia kujitumia katika kutekeleza jukumu lao kuu la
Utoaji haki nchini.
Kwa upande wake,
Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji Mstaafu, Harold
Nsekela ametoa wito kwa watumishi wote kuzingatia maadili ya utumishi kwa
kufuata misingi na taratibu zilizopo.
“Binafsi nimepokea
uteuzi huu kwa moyo mkunjufu, hivyo nimtake kila Kiongozi/ Mtumishi kuzingatia
maadili ya kazi kwani suala la maadili ni la kila mtu,” alisisitiza, Jaji
Nsekela.
Wahe. Majaji wateule (wenye majoho mekundu), Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Naibu Mwenyekiti (NEC) pamoja na Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma, wakisubiri kuapishwa, wa kwanza kulia ni Mhe. Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, wa tatu kulia ni Mhe. Jaji Harold Nsekela, Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma, katikati ni Mhe. Rehema Mkuye, Jaji mteule wa Mahakama ya Rufani, wa tatu kushoto ni Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Jaji mteule wa Mahakama ya Rufani (T), wa pili kushoto ni Mhe. Dkt. Gerald Ndika, Jaji Mteule, Mahakama ya Rufani (T), wa kwanza kushoto ni Mhe. Jackobs Mwambegele, Jaji mteule Mahakama ya Rufani (T).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Wahe. Majaji kabla ya kuapishwa.
Salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisaliama na wateule kabla ya kuapishwa kwao rasmi, aliye nyuma ni Waziri wa Utumishi wa Umma, Mhe. Angela Kairuki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage akila kiapo.
Mhe. Rais akimuapisha Makamu Mwenyekiti, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe.Jaji Hamid Mahamoud Hamid.
Mhe. Rais akimuapisha, Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela, Mhe. Jaji Nsekela anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Mstaafu, Salome Kaganda.
Mhe. Rais akimuapisha, Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Rehema Mkuye, aliyesimama kulia kwa Mhe. Rais ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman.
Mhe. Jaji Mkuye akila kiapo.
Mhe. Rais akimuapisha Jaji Mteule, Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Sivangilwa Mwangesi.
Mhe. Rais akimuapisha Jaji Mteule, Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Dkt. Gerald Ndika.
Jaji Mteule- Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Jackobs Mwambegele akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Wahe.Majaji wateule wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania.
Mhe. Rais (katikati), Waziri Mkuu (wa nne kulia), Mhe. Jaji Mkuu (wa nne kushoto), Jaji Kiongozi Mahakama kuu ya Tanzania (wa kwanza kushoto), Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wateule wa Mahakama ya Rufani (T), na baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu walioshiriki katika hafla fupi ya uapisho iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa Kassim (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe.Hussein Kattanga, muda mfupi baada ya hafla fupi ya Uapishwaji wa Wahe.Majaji.
Baadhi ya Watendaji wa Mahakama na
Wizara walioshiriki katika hafla ya Kuapishwa kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na
Majaji wa Mahakama ya Rufani (T), wa kwanza kulia ni Mhe. Amon Mpanju, Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu,
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, katikati ni Msajili Mkuu, Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, wa pili kushoto ni Mtendaji, Mahakama Kuu
ya Tanzania, Mhe. Sollanus Nyimbi, na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi-Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni