Mhandisi-Ujenzi,
Mahakama ya Tanzania, Bw. Khamadu Kitunzi wa kwanza kushoto akifafanua jambo kwa wageni kutoka
Ethiopia walipotembelea Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kuangalia na kupata
uelewa juu ya ujenzi wa gharama nafuu, wa kutumia teknolojia ya Moladi, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Wakala ya Takwimu nchini Ethiopia, Bw. Biratu Yigezu, wa pili kulia ni Mratibu wa Mradi ujulikanao kama "Statistical for Results Project" SFR uliopo nchini Ethiopia unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, wa pili kushoto ni Msanifu Majengo Mkuu kutoka Wakala wa Takwimu nchini Ethiopia, Bw. Zewdie Shiferaw.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwami na Mahakama ya Wilaya Kibaha, moja kati ya majengo yaliyojengwa kwa teknolojia ya Moladi, jengo hili ni miongoni mwa majengo sita ya Mahakama iliyojengwa/yanayojengwa kwa kutumia Teknolojia ya Moladi, miradi ya ujenzi wa Mahakama inayojengwa kwa kutumia tenolojia hii ya gharama nafuu ni pamoja na Mahakama ya Mwanzo/Wilaya, Bagamoyo, Mahakama ya Mwanzo/Wilaya Mkuranga na Mahakama ya Wilaya-Kigamboni.
Wakiendelea kukagua jengo la Mahakama ya Wilaya- Bagamoyo, inayojengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi.
Dkt. Daniel Mbiso, kutoka Chuo cha Ardhi akitoa mada juu ya Teknolojia ya Ujenzi wa gharama nafuu- Moladi Tanzania kwa wageni kutoka Ethiopia waliotembelea Mahakama nchini kwa lengo la kuangalia na kukagua miradi ili kupata utaalamu juu ya teknolojia hii ya ujenzi.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya Bagamoyo, linaloendelea na ujenzi kwa kutumia teknolojia ya Moladi.
Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw.Sollanus Nyimbi akieleza jambo kwa wageni kutoka Ethiopia walipotembelea katika Mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Mkuranga mapema jana, wa tatu kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya-Mkuranga.
Mkurugenzi wa MOLADI Construction Tanzania, Bw. Abeid akiwaeleza jambo wageni kutoka Ethiopia walipotembelea katika jengo la Mahakama ya Wilaya Mkuranga linaloendelea kujengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi.
Wageni kutoka Wakala wa Takwimu nchini Ethiopia(Central Ethiopian Statistical Agency-CSA) wakiwa katika jengo la Mahakama ya Wilaya Mkuranga linaloendelea na ujenzi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu, Bw. Biratu Yigezu, kushoto ni Msanifu Mkuu wa Majengo-CSA, Bw. Zewdie Shiferaw na kulia ni Mratibu wa Mradi wa "Statistics for Results" uliopo nchini humo, Bw. Jemal Mohammed.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kigamboni linaloendelea kujengwa kwa teknolojia ya Moladi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni