Baadhi ya wazee kutoka kata ya Zingiziwa wakitoa malalamiko
yao katika banda la Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora leo, wakati
wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na yameshirikisha wadau
mbalimbali wa Mahakama.
Kaimu Mkurugenzi Elimu
kwa Umma na Mafunzo kutoka Tume ya Haki za Binadamu, Alexander Hassan
akimsikiliza mzee Kassium Mwesimba wakati akitoa lalamiko lake leo kwenye banda la Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma za matibabu ya afya
leo kwenye Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
|
Daktari Natalius
Kapilima kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala (Amana) akimpima
mwananchi aliyefika kupata ushauri
wa huduma za afya kwenye Banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mhandisi Khamadu
Kitunzi kutoka kitengo cha majengo cha Mahakama ya Tanzania, akitoa
maelezo kuhusu teknolojia ya ujenzi
wa nyumba wa gharama nafuu ijulikanayo kwa jina la Moladi kwa fundi ujenzi,
Charles Kang’ombe mkazi wa Ilala, jijini
Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni