Mtendaji Mkuu Mahakama ya
Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akifungua mafunzo Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kwa Maafisa TEHAMA kutoka Mahakama
Kuu ya Tanzania . Mafunzo hayo ni ya muda wa wiki moja yenye
lengo la kuongeza ujuzi yameanza leo tarehe 16.01.2017 katika jengo
la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na
yanafanywa na Mahakama ya Tanzania kwa ushirikiano wa Wakala ya
Serikali Mtandao(eGA), yatamalizika Januari, 20, 2017.
| ||||||||||
Mtendaji Mkuu Mahakama ya
Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akifungua mafunzo Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kwa Maafisa TEHAMA kutoka Mahakama
Kuu ya Tanzania . Mafunzo hayo ni ya muda wa wiki moja yenye
lengo la kuongeza ujuzi yameanza leo katika jengo la Shule
ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na yanafanywa na
Mahakama ya Tanzania kwa ushirikiano wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA).
Wataalamu wa IT wakimsikiliza Mtendaji Mkuu- Mahakama ya Tanzania alipokuwa akifungua mafunzo.
|
Baadhi ya Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakiwa katikamafunzo ya muda wa wiki moja kuhusu
kuwajengea uwezo na ujuzi kwenyemasuala ya TEHAMA yaliyoanza leo katika jengo la
Shule ya Sheria lililopo Sinza,
Kijitonyama jijini Dares Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa kwa ushirikiano wa wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA).
Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais,
Utumishi na Utawala Bora, Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari akitoa
mada juu ya Serikali Mtandao wakati wa mafunzo
ya Maafisa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania.Mafunzo hayo ni ya muda wa wiki moja yameanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama
jijini Dares Salaam na yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama na Tanzania Wakala
ya Serikali Mtandao (eGA).
Mkurugenzi Msaidizi- TEHAMA, Mahakama ya Tanzania, Bw. Machumu Essaba (aliyesimama) akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mtendaji Mkuu, kufungua rasmi Mafunzo ya wiki mmoja ya Maafisa TEHAMA kutoka Kanda zote za Mahakama nchini. (Picha na; Mary Gwera)
Na, Magreth Kinabo
Mtendaji Mkuu
Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga amewataka Maafisa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania kutumia elimu na ujuzi
ili kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye masuala ya TEHAMA.
Kauli hiyo
imetolewa na Mtendaji huyo wakati akifungua mafunzo hayo ya muda wa wiki
moja yaliyoanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo
Sinza, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambayo yanafanywa kwa
ushirikiano wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(eGA).
“Mnatakiwa kutumia
elimu mliyonayo , ujuzi mtakaoupata ikiwemo kuwa wabunifu katika
vitu vipya ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifumo ya
TEHAMA, alisema Mtendaji Mkuu, Bw. Kattanga.
Aliongeza kuwa
maafisa hao wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano
ili kuwezesha
kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa pamoja kwenye
shughuli za mifumo ya TEHAMA. Pia aliwataka kutumia ujuzi watakaoupata
kuwafundisha wengine.
Bw. Kattanga
aliwataka maafisa hao kuwa na uweledi katika ya masuala ya Serikali
Mtandao, kujituma kufanya kazi na kuacha tabia ya kulalamika
,ikiwemo kuwa na mtandao wa kubadilishana mawazo katika masuala ya
kitaaluma.
Akitoa mada kuhusu
Shughuli za Wakala ya Serikali Mtandao, Dkt. Bakari alisema
dhima yake ni kusogeza huduma za Serikali kwa wananchi kupitia
dirisha moja, ili kuwezesha utendaji wa shughuli hizo kwa gharama
nafuu , ubora , wakati na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Alisema mfumo huo pia unasaidia kuboresha huduma
za Serikali katika jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni