Jumapili, 15 Januari 2017

MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO AFUNGA RASMI MAFUNZO YA UTUNZAJI KUMBUKUMBU KWA NJIA ZA KIELEKTRONIKI YALIYOTOLEWA KWA MAAFISA TEHAMA NA WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU WA MAHAKAMA


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika akitoa neno alipokuwa akifunga rasmi Mafunzo ya Wiki yaliyotolewa kwa baadhi ya Maafisa TEHAMA na Wasaidizi wa Wakumbukumbu juu ya Utunzaji wa Kisasa/Kielektroniki wa Kumbukumbu za Mahakama, katika Mafunzo hayo Mada mbalimbali zilitolewa zote zikilenga katika kuwawezesha kuhifandi kumbukumbu kwa njia za Kielektroniki, kulia ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Bw. Fahamu Mtulya.
Mkuu wa Wilaya akiendelea kuzungumza na Wanasemina katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, yaliyofungwa rasmi Januari 13, 2017.
 Baadhi ya Wasaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama pamoja na Maafisa TEHAMA wakiwa katika Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA-Lushoto.
Wanasemina.
 Mmoja kati ya Wanasema akipatiwa/ akitunukiwa Cheti cha kuhitimu Mafunzo hayo ya Wiki mbili, katika hafla hiyo fupi ya kufunga Mafunzo, Mhe. Mkuu wa Wilaya aliwatunuku vyeti Washiriki wote wa Mafunzo hayo.
 Mshiriki akipatiwa cheti chake na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto.
 Washiriki wakiendelea kupokea vyeti vyao.
Mshiriki wa Mafunzo akipokea cheti.

Baadhi ya Washiriki wakipokea vyeti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. January Lugangika.
Meza Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo yaliyofungwa rasmi Januari 13, 2017 , Chuo cha Uongozi wa Mahakama-IJA- Lushoto.
Picha ya pamoja na Washiriki.
Aidha katika hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo, Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Maafisa TEHAMA pamoja na Wasaidizi wa Kumbukumbu walioshiriki katika mafunzo hayo kuwa chachu ya ya ufanisi katika utendaji kazi.
"Naomba niwasisitize washiriki wote uwa mafunzo haya mliyoyapata ya utunzaji wa kisasa wa Kumbukumbu Kielektroniki mna wajibu mkubwa wa kufanyia kazi mafunzo hayo kivitendo huko muendako na muendelee kuwa na nidhamu na nidhamu na uadilifu ili kurejesha imani ya jamii dhidi ya Mahakama," alisisitiza Mhe. Lugangika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni