Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma akiwa tayari kwa hafla ya kuapishwa leo
Ikulu jijini Dar es Salaam.
|
Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe.
Mohamed Chande Othman, kabla ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
|
Baadhi ya viongozi wa
Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja hafla ya kuapishwa Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania na leo Ikulu jijini
Dar es salaam.
|
Baadhi ya viongozi wa
Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja hafla ya kuapishwa Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania na leo Ikulu jijini
Dar es salaam.
|
Baadhi ya viongozi wa
Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja hafla ya kuapishwa Kaimu
Jaji Mkuu wa Tanzania na leo Ikulu jijini
Dar es salaam.
(Picha na Magreth Kinabo na Mary Gwera)
|
Na Magreth Kinabo
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo, Januari 18, mwaka huu
amemwapisha Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma.
Rais Magufuli
alimwapisha Jaji Mkuu huyo katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, ambayo ilihudhuriwa na
baadhi ya viongozi wa wakuu wa Serikali na Mahakama ya Tanzania, wakiwemo
majaji.
Miongoni wa viongozi
wakuu wa Serikali walihohudhuria Makamu wa Rais, Mhe. Samia Hassan Suluhu, Jaji
Mstaafu, Mhe. Mohamed Othman Chande na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi, John
Kijazi pamoja na viongozi wengine wa Mahakama ya Tanzania.
Akizungumza baada ya
kuapishwa na Rais Magufuli, Kaimu Jaji Mkuu
huyo, alisema atahakikisha Mahakama nchini zinatumia mfumo wa Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao utarahisisha utendaji kazi wa shughuli
za Mahakama na kuwezesha haki za wananchi zipatikana kwa wakati kwa faida ya maedeleo
ya nchi.
“Mpango huu wa matumizi
ya TEHAMA hii itawezesha haki kutendeka kwa wakati,” alisema Profesa Juma.
Aidha, Kaimu Jaji Mkuu
huyo anachukua nafasi ya Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.
Kabla ya kuteuliwa
katika wadhifa huo, Profesa Ibrahim Juma, alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani
Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni