Alhamisi, 20 Aprili 2017

VIONGOZI WA MAHAKAMA YA TANZANIA NA TAKUKURU WAJADILIANA KUHUSU KITUO CHA HUDUMA YA SIMU CHA DHARURA.


Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na  Rushwa (TAKUKURU), Ekwabi Mujungu (kulia)(wakiwa  katika picha  ya pamoja  mara kumaliza  kikao kazi kati ya uongozi wa taasisi hiyo  na  baadhi ya viongozi  wa Mahakama ya  Tanzania, kilichofanyika  kwenye ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo. (katikati)  Mkurugenzi Msaidizi  wa  na Usimamizi wa .  Kushoto ni wa Kitengo cha Maboresho  wa Mahakama ya Tanzania, Zahra  Maruma.

Jumla  ya sh. 66 zimetumika katika kukarabati   chumba cha kisasa kwa ajili ya kuandaa  Kituo cha Huduma   cha  Simu cha  ya Dharura, ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma  za serikali kwa wananchi.
Hayo yalisemwa  leo tarehe 20.04.2017  na Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na  Rushwa (TAKUKURU), Ekwabi Mujungu wakati wa kikao kazi ya uongozi wa taasisi hiyo  na  baadhi ya viongozi  wa Mahakama ya  Tanzania, kilichofanyika  kwenye ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo.
Bw. Mujungu alisema   wananchi wamekuwa wakitumia njia ya kutuma ujumbe kwa njia ya simu hiyo namba 133 na kuzungumza na wataoa huduma, kwa ajili ya kuuliza swali, kutuma taarifa au maoni kuhusu mapambano dhidi ya  rushwa.
“ Kutoa  taarifa   za watu  wanaojihusisha na vitendo vya rushwa kwa kupiga  nambari *113# na kufuata maelekezo,” alisema Mujungu.
 Aliongeza kwamba  ofisi hiyo inafanya kazi kwa muda wa saa 24 na kuna watumishi  14 waliopangwa  maalum kwa ajili ya kazi hiyo.
Naye Mratibu  wa kituo hicho, Doreen Kwapani alisema tangu wanzishe huduma hiyo  Mei 2016 hadi Machi , 2017 jumla ya wananchi 268,708 wametumia huduma  hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Maboresho  wa Mahakama ya Tanzania, Zahra  Maruma aliushukuru uongozi  wa taasisi  hiyo kwa ushirikiano waliounyesha na kuongeza kwamba taasisi hizo zitaendelea kushirikiana.

Mkuu wa Kitengo cha Maboresho  cha Mahakama ya Tanzania, Zahra Maruma(kushoto) akimkabidhi  jarida la Mpango Mkakati wa Miaka Mitano  wa Mahakama ya Tanzania, Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Ekwabi  Mujungu (kulia) katika kikao kazi  cha kubadilisha uzoefu juu ya Kituo cha Simu  cha  Huduma  ya Simu ya Dharura cha Taasisi hiyo kilichofanyika leo tarehe 20.04.2017.
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na  Rushwa (TAKUKURU) wa pili (kushoto)wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na  watumishi wa Mahakama ya Tanzania, wakiwemo  wa Taasisi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni