Ijumaa, 21 Aprili 2017

RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI AMTEMBELEA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA


  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akiwa na Mgeni wake ambaye ni Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki (East Africa Court of Justice) Mhe. Jaji Dkt. Emmanuel Ugirashebuja alipomtembelea ofisini kwake leo jijini 
Dar es salaam


KAIMU JAJI MKUU AKUTANA NA RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI

Na Lydia Churi-MAHAKAMA 

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki (East African Court of Justice).  

Akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mhe. Jaji Dkt. Emmanuel Ugirashebuja aliyemtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam, Kaimu Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania itashirikiana na Mahakama ya Afrika Mashariki hasa katika eneo la uboreshaji wa teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa mashauri.

Alisema hivi sasa Mahakama ya Tanzania inaendelea na maboresho pamoja na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata haki kwa wakati. Aliongeza kuwa ili kufikia lengo hilo, pamoja na mambo mengine, Mahakama imekuwa ikiwapatia mafunzo ya mara kwa mara Majaji na Mahakimu.

Kwa upande wake, Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki alizitaka Mahakama za Afrika Mashariki kushirikiana ili wananchi wake waweze kupata haki zao.

Aidha, Rais Ugirashebuja alielezea kufurahishwa kwake na hatua ya Mahakama ya Tanzania ya kuwaalika Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki kushiriki kwenye Mafunzo mbalimbali kwenye chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto. 

Dkt.Ugirashebuja aliishukuru Mahakama kwa ushirikiano huo na kuahidi kuuendeleza.
  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akiwa na Mgeni wake ambaye ni Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki (East Africa Court of Justice) Mhe. Jaji Dkt. Emmanuel Ugirashebuja mara baada ya kufanya mazungmzo leo jijini Dar es salaam
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma (katikati) akiwa na wageni wake walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akiwa na wageni wake walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Mahakamaya Rufani Mheshimiwa John Kahyoza.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akiwa na wageni wake walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Mahakamaya Rufani Mheshimiwa John Kahyoza. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni