Jaji
Mkuu wa Tanzania akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Theresia
Mahongo wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa
Mahakama ya Mwanzo, Karatu. Uwekaji wa jiwe hilo la msingi uliohudhuriwa na
Watumishi wa Mahakama, Wananchi, Viongozi wa dini, Maafisa kutoka serikalini
n.k, anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi.
Ujenzi
wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo Karatu mjini ulianza mnamo Mwezi wa
Novemba Mwaka 2012 kwa nguvu za wananchi kwa kuhamasishwa na Mkuu wa Wilaya
pamoja na Hakimu wa Wilaya Mfawidhi. Aidha, thamani ya mradi huo wa umaliziaji wa
jengo la Mahakama ya Mwanzo Karatu Mjini ni kiasi cha Fedha za Kitanzania
Shilingi Milioni Mia Moja Thalathini na Saba Mia Mbili Sabini na Tano Elfu na
Mia Tano Arobaini 137,275,540/=
Meza Kuu ikiwa katika hafla ya uwekaji jiwe la Msingi katika jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo Karatu iliyopo mkoani Arusha.
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akitoa risala katika
hafla hiyo fupi iliyohudhuriwa na wananchi wa mji wa Karatu, katika risala yake
Mhe. Jaji Juma amewashukuru wananchi wa Wilaya hiyo kwa kujitoa kwa ujenzi wa
Mahakama hiyo na kuwataka wananchi wengine kuwa na moyo huo ili Mahakama kwa
kushirikiana na Wananchi kufikia azma ya kila kata kuwa na Mahakama ya Mwanzo.
Makundi mbalimbali ya wananchi walioshiriki katika hafla hiyo
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akikagua jengo la Mahakama ya Mwanzo Karatu aliloliwekea jiwe la msingi, mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Theresia Mahongo, mwenye tai nyekundu ni Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mhe. Mukama. (picha na Mary Gwera, Karatu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni