Alhamisi, 11 Mei 2017

MAHAKAMA YA RUFAA YAANZA KUSIKILIZA OMBI LA RUFAA LA KESI YA WASSIRA DHIDI YA BULAYA.


Aliyekuwa  kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Steven  Wassira  akiwa katika jengo la Mahakama ya Rufaa jijiji Dares Salaam akizungumza jambo na baadhi ya mawakili kabla ya kusikiliza kwa Rufaa ya kesi yake dhidi ya Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya.  Katika kesi hiyo jopo la majaji watatu  wa Mahakama ya Rufaa limepanga kuendelea na kesi hiyo Jumatatu ijayo ya Mei 15, mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa  leo  Mei 11, mwaka huu katika Mahakama hiyo  baada ya  Pande zote mbili  kutoa maelezo  ya sababu za rufaa.








Wakili wa Mbunge  wa Jimbo la Bunda Mjini, Tundu Lissu  akizungumza  jambo na mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na  wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga  hukumu ya  Mahakama Kuu Kanda ya  Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.

(Picha  na Magreth Kinabo)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni