Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya
Hakimu Mkazi/Mkoa Arusha, Mhe. Desdery Kamugisha akimuonesha moja ya jengo
chakavu la Mahakama ya Mwanzo, Maji ya Chai Arusha pindi Mhe. Kaimu Jaji Mkuu
alipotembelea kwa lengo la kukagua jengo hilo,mapema Mei 11 mwaka huu.
Hakimu Mfawidhi,Mahakama ya Wilaya Arumeru akimsomea taarifa ya hali ya utendaji kazi katika Mahakama hiyo Mhe. Kaimu Jaji Mkuu pindi alipotembelea Mahakama hiyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Kanda ya Arusha.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Prof. Ibrahim Juma akisamiliana na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha
alipowasili katika viwanja vya Mahakama Kuu-Arusha kukamilisha ziara yake ya
siku mbili mkoani humo.
Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi,
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mhe. Kamugisha akimsomea taarifa ya hali ya
utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo. Lengo la ziara ya Mhe. Kaimu Jaji
Mkuu katika Kanda hiyo ni kujifunza na kuona hali halisi ya mazingira ya kazi
na utekelezaji wa majukumu.
Naibu
Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Rumisha (wa kwanza kulia) akimuonesha
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, moja ya kumbi za Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha pindi
alipokuwa akikagua ofisi mbalimbali za Mahakama ya Mkoa na Mahakama Kuu katika
Kanda hiyo.
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Juma akiwa katika Kompyuta Mpakato akikagua Mfumo wa
Kuratibu takwimu za Mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS) kuhakikisha kama
inafanya kazi ipasavyo, pembeni ni Afisa TEHAMA, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha,
Bw. Athuman.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania,
akiongea na Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama (hawapo pichani), katika
maongezi yake na Watumishi hao Mhe. Jaji Prof. Juma amewataka na kuwasisitiza
Watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ikiwa ni pamoja na kuwa na
lugha nzuri kwa Wateja/Wananchi wanaowahudumia. kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha na kushoto ni Mhe. Rumisha, Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama
wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza nao.
Watumishi wamkimsikiliza kwa makini Mhe. Kaimu Jaji Mkuu (hayupo pichani)
Mtendaji, Mahakama Kuu-Arusha, Bw. Edward Mbara akiwasilisha taarifa ya hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo mbele Mhe. Kaimu Jaji Mkuu na Watumishi wa Mahakama, katika taarifa yake Bw. Mbara alikiri kuwa Kanda ya Arusha inakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu chakavu ya majengo ya Mahakama n.k (picha na Mary Gwera,Arusha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni