Jumanne, 16 Mei 2017

MAHAKAMA YA KIBAHA YAPATA VIFAA VYA KISASA VYA TEHAMA

Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya-Pwani imepata vifaa vya kisasa vya TEHAMA, vifaa hivyo vya kisasa kabisa ambavyo vimetolewa  na Benki ya Dunia tayari vimeshawasilishwa katika Mahakama hiyo.

Vifaa viliwasilishwa katika Mahakama hiyo mapema Mei 12, ambapo vitaifanya Mahakama hiyo iwe ya kisasa na ya mfano kwa utumiaji wa vifaa vya TEHAMA.

Viongozi na Watumishi wa Mahakama hiyo wamefurahi kupatiwa vifaa hivyo na wameomba vifaa hivyo vianze kutumika haraka iwezekanavyo ili kwenda sambasamba na Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Vifaa hivyo vya kisasa kabisa vitawezesha Mahakama hiyo kupokea ushahidi mubashara wakati shauri likiendelea Mahakamani hata kama shahidi hayupo moja kwa moja Mahakamani.

Zifuatavyo ni baadhi ya picha zinazoonesha upokeaji wa vifaa hivyo;
'Standby Generator' likishushwa tayari kwa kufungwa katika Mahakama hiyo ambayo imepata vifaa vya Kisasa vya TEHAMA.
Pichani ni muonekano wa Maafisa wa Mahakama kutoka Makao Makuu wakikabidhi vifaa hivyo.
Moja ya Mtumishi wa Mahakama Mkoani Pwani akiangalia kwa umakini vifaa hivyo.
Vifaa vikiendelea kushushwa.

Afisa kutoka Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi-Mahakama 'JDU', Bw. Haroun Tungaraza akishiriki katika ushushaji wa vifaa hivyo vya TEHAMA ambavyo vimetolewa kwa ufadhili wa Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Mahakama unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Muonekano wa Maboksi yenye vifaa vya ICT vilivyowasilishwa katika Mahakama hiyo, mkoani Pwani.
Muonekano wa jengo la Mahakama hiyo ambayo vifaa hivyo vya TEHAMA vimepelekwa. Mahakama hiyo ya mfano ilizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Septemba 23, 2016.
Katika kutekeleza huduma zake, moja ya vipaumbele vya Mahakama ni pamoja na kufanya matumizi ya TEHAMA kuwepo Mahakamani ili kurahisisha huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

Maoni 2 :

  1. Mahakama mnakwenda kwa speed nzuri. Tulidhani mtaishia DSM lakini tunaona hata Mikoani pia mnafanya maboresho

    JibuFuta
  2. Tunashukuru kwa Pongezi, tunaahidi kuendelea kuboresha huduma ya Utoaji haki nchini kwa manufaa ya Umma.

    JibuFuta