Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Ferdinad Wambali amesema kwamba mkoa wa
Kigoma utapatiwa Mahakama Kuu hivi
karibuni,ikiwa ni hatua ya kuwaondolea
adha wanaoipata wananchi ya kutafuta huduma ya mahakama hiyo kutoka eneo moja hadi jingine.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki
iliyopita na Jaji Kiongozi wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya ya Kibondo kuhusu malengo ya
ziara yake katika mkoa wa Kigoma, hivyo aliwataka baadhi
ya viongozi na wananchi kuvuta subira.Jaji Kiongozi , pia alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, wakiwemo baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu kutoka kanda hiyo ambayo inajumuisha mikoa miwili yaani na Tabora na Kigoma.
“Tayari kiwanja kimeshapatikana na eneo la Buhigwe na tenda imeshatangazwa, hivyo mchakato wa
ujenzi utaanza hivi, karibuni,”alisema Jaji Kiongozi.
Kiwanja hicho
kina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 16,000. Mkoa huo,
unahitaji huduma ya Mahakama Kuu kwa sababu ya kukua kwa idadi
ya watu,pia hivi sasa watu wanatoka
katika mkoa huo kwenda kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoa wa Tabora , pia kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Jaji Kiongozi
aliongeza katika kanda hiyo, wilaya ambazo hazina mahakama za wilaya zitajengewa mahakama kwa
kuwa Mahakama ya Tanzania kupitia mpango
Mkakati wa Miaka Mitano(2015/16 hadi 2019/20
imejipanga kujenga mahakama kila wilaya, tarafa na kata.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe, Ferdinand Wambali (aliyekaa
katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya viongozi wa Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Tabora
na Shinyanga baada kulitembelea
jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga Juni, 26,mwaka huu, ambapo alifanya ukaguzi wa shughuli za utendaji kazi na miundombinu ya Mahakama hiyo. Wengine ni baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Shinyanga.
Picha ya muonekano wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya
Shinyanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni