Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma akizungumza na baadhi
ya waandishi wa habari mara baada ya kuwapokea
Mawakili wapya 248 walioapishwa na kukubaliwa leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Magreth Kinabo)
Na Magreth Kinabo
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma,
amewataka mawakili kufanya kazi kwa kuangalia sheria za nchi na za kimataifa ili kuweza kuwasaidia Watanzania katika masuala
yanayohusu sheria hususan wananchi wanyonge ili nchi iweze kufikia malengo ya kimaendeleo .
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Jaji Mkuu huyo, wakati wa hafla fupi ya 56 (1986-2017)
ya kuwakubali na kuwaapisha Mawakili wapya 248 iliyofanyika leo kwenye Kiwanja cha Mahakama Kuu kilichopo jijini Dar es Salaam.
“Leo tumewaapisha
Mawakili waliokubaliwa, nilifanya nao mazungumzo kila mmoja, wengi wao ni
vijana wadogo wenye miaka 25 hadi 30 ya kufanya kazi ya sharia, hivyo kukubaliwa kwao sio mwisho wa kusoma wanapaswa kusoma
sheria za kimataifa ili kufahamu
sheria za utaratibu wa nchi zingine,” alisisitiza .
Profesa Juma aliwataka Mawakili hao, waendelee kufanya kazi kwa
weledi, kuzingatia maadili na kuepuka
kujiingiza katika vitendo vya rushwa,kwa sababu bado
wananchi wana hisia kwamba
tatizo la rushwa ni kubwa ndani ya Mahakama ya Tanzania.
"Wazazi na Serikali imetumia gharama
kubwa kuwasomesha, hivyo watambue mchango huu, waisaidie
Serikali na wazazi wao ili Tanzania
isonge mbele, alisisitiza.
Akijibu swali lililoulizwa na baadhi ya waandishi kuhusu kuwepo kwa tetesi
kwamba Chama cha Mawakili Tanzania (TLS) kinaweza kufutwa, Kaimu jaji Mkuu alisema sheria ikitungwa haitalenga mtu wala taasisi, hivyo hofu hiyo haina sababu kuwepo
kwa kuwa Mawakili ni sehemu ya Mahakama.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni