Ijumaa, 30 Juni 2017

MAHAKAMA YA TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA 41 YA BIASHARA YA KIMATAIFA- SABASABA

  Banda la Maonesho la Mahakama ya Tanzania kama linavyoonekana kwa mbele. Mahakama inashiriki Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yaliyoanza Juni 28-Julai 8, 2017, katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.
  Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Joachim Tiganga akimuelimisha mwananchi aliyetembelea banda la Mahakama katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yaliyoanza Juni 28-Julai 8, 2017, katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

 Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Joachim Tiganga akiwaelimisha wananchi waliotembelea banda la Mahakama katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yaliyoanza Juni 28-Julai 8, 2017, katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.
  Afisa wa Mahakama ya Rufaa kitengo cha Mirathi, Rukia Idrisa akisubiri kuhudumia wananchi wanaotembelea banda la Mahakama ya Tanzania.

 Baadhi ya Watumishi wa Mahakama wakiwa tayari kuhudumia wananchi katika Maonesho ya Sabasaba  
 Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto iliyoko Kisutu jijini Dar es salaam  Mhe. Devotha Kissoka (Kushoto) akiwa katika Banda la Mahakama tayari kwa kuelimisha Wananchi watakaotembelea banda la Mahakama masuala Mbalimbali yahusuyo Mahakama Maalum ya Watoto.
  Baadhi ya Watumishi wa Mahakama pamoja na wadau wakielekezana jambo katika banda la Maonesho jana.  
  Msajili wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Eddy Fussi akisubiri kuwahudumia wananchi wanaotembelea banda la Maonesho la Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yaliyoanza Juni 28-Julai 8, 2017, katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

 Picha na Lydia Churi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni