Na Magreth Kinabo
Mahakama ya Tanzania imeshika nafasi ya tatu katika daraja lililohusisha taasisi za serikali zinazotoa huduma zilizoshiriki kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya sabasaba vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, vilivyoko Barabara ya Kilwa.
Washindi wa Maonesho hayo walitangazwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Maonesho uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo katika viwanja vya sabasaba.
Aidha, katika Maonesho hayo, nafasi ya kwanza ilishikwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Akizungumzia kuhusu ushindi wa nafasi hiyo, kwa Mahakama ya Tanzania, Mmoja wa Waoneshaji kwenye Banda la Mahakama ya Tanzania, ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Mhe. Joachim Tiganga, alisema siri ya ushindi huo ni kitendo cha mahakama kujipanga kuanzia Mahakama za Mwanzo hadi Mahakama ya Rufani.
Aliongeza
kwamba jambo lingine lililosaidia ushindi huo, ni Mahakama kujipanga pamoja na Divisheni
zake zote nne yaani Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mahakama Kuu Divisheni
ya Biashara, Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi na Mahakama Kuu
Divisheni ya Kazi.
"Tuna pia wawakilishi wa Mahakama za Mikoa, Mahakama za Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopo jijini Dar es Salaam. Tuna
vitengo pia , ambavyo ni Kitengo
cha Usuluhishi cha Mahakama Kuu,
Kitengo cha Mirathi, Kitengo cha Usimamizi
wa Maboresho ya Mahakama, Kitengo cha Utawala na Utumishi, Kitengo cha TEHAMA na
Kurugenzi ya Malalamiko na Maadili, alifafanua Mhe. Tiganga.
Aliongeza kwamba
jambo lingine lililochangia ushindi huo,
ni kuwepo kwa taarifa sahihi kwenye kumbukumbu za Mahakama ya Tanzania.
“ Tumemwezesha kila mtu yoyote
mwenye shida anawe za kupata
majibu ya hoja yake katika Banda la Mahakama ya Tanzania ,
Mfano Mfumo wa Kusajili
kesi Kielekroniki. Kila
banda linasimamiwa na mtu
nafasi ya weledi wa kutosha na TEHAMA, na Mkurugenzi ” alisisitiza
Tiganga.
Wadau wanaoshiriki katika banda la Mahakama ya Tanzania, ni Chama cha Mawakili Tanzania(TLS), Chuo cha
Mahakama Lushoto, Chama cha Majaji Wanawake
(TAWJA), Tume ya Kurekebisha Sheria na Kamisheni ya Usuluhishi.
Afisa TEHAMA wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ahmed Mbilinyi akifafanua masuala kuhusu taaluma hiyo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Mahakama ya Tanzania, Kitengo cha TEHAMA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni