Na Magreth Kinabo
Viongozi wa Mahakama za Mwanzo, Hakimu Mkazi na Mahakama
za Wilaya watakiwa kuhakikisha kwamba wanailinda viwanja
vya Mahakama ya Tanzania na kuviwezesha kupata
hati miliki ili
kuwezesha upanuzi wa miundombinu
ya Mahakama ikiwa ni hatua kuendelea kusogeza huduma za Mahakama kwa
wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa
na Jaji Kiongozi Mahakama ya Kuu ya
Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali
alipokuwa akizungumza na baadhi ya
viongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora na watumishi
kwenye ziara ya siku tatu iliyoanza tarehe 19.06 2017 na kumalizika tarehe 22.06.2017.
Mhe . Jaji Kiongozi
alisema hayo, katika ziara hiyo
yenye lengo la kukagua
shughuli za utendaji kazi wa Mahakama sanjari na kuendelea kutoa elimu
ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015/16
hadi 2020) wa Mahakama ya Tanzania, kwa
Viongozi na watumishi wa Mahakama,
Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanry Wakuu
wa Wilaya, wakiwemo wajumbe wa Kamati
za Ulinzi na Usalama za Mkoa huo.
“ Hakikisheni mnaweka uzio kwenye mipaka ya viwanja vya mahakama na
kutafuta hati miliki na kuweka uzio, kwa sababu
viwanja vina maeneo makubwa , hivyo rasilimali muhimu ambazo zitatumika kupanua miundombinu ya mahakama
bila vikwazo,” alisema Mhe. Jaji Kiongozi.
Aidha Mhe. Wambali
aliwaomba watumishi wa Mahakama,
ambao wanaofanya kazi katika miundombinu isiyoridhisha kutokata tamaa ya
utendaji kazi, bali waendelee kufanya
jitihada hizo ili kuhakikisha malengo ya mpango mkakati huo wa Mahakama
yanafanikiwa.
Pia alimtaka
kila mtumishi wa Mahakama kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, kuzingatia
kanuni za utumishi wa umma na maadili, ukiwemo ubunifu bila kujali nafasi
aliyonayo.
Mpango huo, mkakati una nguzo kuu tatu, ambazo ni Uimarishaji wa
Utawala Bora, Uwajibikaji na Usimamizi wa Rasilimali,Upatikanaji wa Haki kwa Wakati,na Ushirikishwaji wa wananchi na
wadau katika shughuli za Mahakama.
Katika ziara
hiyo Mhe. Wambali alitembelea Mahakama
za Mwanzo, Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na Mahakama Kuu,katika
Wilaya za Igunga, Nzega, Sikonge , Uyui, Kaliua, Tabora
na Urambo ambapo aliridhishwa kasi usikilizaji wa mashauri kwa sababu
hakuna kesi za muda mrefu kuanzia kipindi cha Januari hadi Mei,mwaka 2017.
|
.
\
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni