Jumanne, 20 Juni 2017

JAJI KIONGOZI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA YA WILAYA YA IGUNGA MJINI.

 


Jaji Kiongozi  wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand  Wambali akipata maelezo  jana kabla  ya kuzindua  jengo la Mahakama ya  Wilaya ya  Igunga Mjini mkoani Tabora , kutoka kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi  wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Mhe. Ajali  Millanzi, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015-2020) wa Mahakama ya Tanzania.  


Jaji Kiongozi  wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand  Wambali akikata utepe  kama ishara ya kuzindua  jengo la Mahakama ya  Wilaya  ya  Igunga Mjini, mkoa wa  Tabora lililojengwa  kwa ushirikiano  wa Mahakama  na wadau, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wa Miaka Mitano(2015/2020).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni