Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim
Juma,(wa pili kulia ) akiwa katika
picha ya mara baada ya kukabidhiwa seti ya vitabu vitano
vya sheria kutoka pamoja na Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee
Haji( wa pili kushoto) kwa Niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar(ambaye
hayupo pichani) na wa kwanza kulia ni Mkuu
wa Kitengo cha Uandishi wa Sheria kutoka Zanzibar, Saleh Mumarak.
Na Magreth
Kinabo.
Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim
Juma, amewataka wanasheria wa Tanzania Bara kujifunza uzoefu
wa kubadilisha sheria mbalimbali
kwa kutumia vitabu vya
sheria kutoka Zanzibar kwa ajili ya
kufanya utafiti na kufundisha katika vyuo vikuu.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 16.06.2017, na
Kaimu Jaji Mkuu huyo, wageni kutoka Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, wakati akizungumza na ujumbe huo mara baada kuwasili katika Ofisi ya Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyopo
jijini Dar es kwa ajili mazungumzo ya kubadilisha uzoefu juu ya
mabadiliko ya vifungu vya sheria mbalimbali.
Ugeni huo, ulikabidhi seti ya vitabu vitano
vilivyobadilishwa kutoka 35, ambapo ulizungumzia kuhusu mabadiliko hayo na masuala
mbalimbali ya Mahakama ya Tanzania.
“Kuna haja ya
kujifunza sheria bora kutoka Zanzibar, ambazo zinaweza kusaidia kufanya tafiti
mbalimbali na kutumika kufundisha kwenye vyuo vikuu.,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Aidha Mhe.
Jaji Kaimu Jaji Mkuu huyo aliushukuru
ugeni huo, kwa kukabidhi vitabu hivyo kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar,Mhe. Omar Makungu.
Akizungumzia kuhusu vitabu hivyo, Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee Haji alisema
vitabu hivyo vilivyokabidhiwa ni mabadiliko
kutoka vitabu vya sheria 35 hadi vitano. Mabadiliko hayo ya kisheria
yamefanyika kutoka mwaka 1980 hadi 2015.
Mhe. Mzee alisema
ofisi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano na kubadilisha uzoefu wa masuala hayo
na mengine ya Mahakama baina ya pande zote mbili .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni