Ijumaa, 16 Juni 2017

KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA AKABIDHIWA SET YA VITABU VITANO VYA SHERIA KUTOKA ZANZIBAR.


Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma,(kulia) akipokea kitabu kimojawapo kutoka kwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee  Haji(kushoto). Vitabu hivyo, vimefanyiwa  mabadiliko  ya kisheria kutoka vitabu  35 hadi  kufikia  vitabu vitano kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 2015.


Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma,(katikati) akipokea kitabu kimojawapo kutoka kwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee  Haji (kushoto) kwa Niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar(ambaye hayupo pichani) na Mkuu wa Kitengo cha Uandishi wa Sheria kutoka Zanzibar, Saleh Mumarak(kulia). 
 

Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma, akizungumza jambo.
 

Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma , akisikiliza  utambulisho wa   wageni  hao, kutoka Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,   baada  ya wageni  hao,(ambao  hawapo pichani) kuwasili  katika Ofisi ya Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyopo jijini  Dar es Salaam leo  kwa ajili  mazungumzo kuhusiana na mambo ya kubadilisha uzoefu  wa kisheria.


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee  Haji,(kulia  wa kwanza) na   akitoa maelezo kuhusu  mabadiliko ya vitabu vya kisheria kutoka 35 hadi vitano kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 2015, kwa Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma, (ambaye  hayupo  pichani ). Kushoto ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. John Kahyoza.


Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee  Haji,(kulia  wa kwanza) na   akitoa maelezo kuhusu  mabadiliko ya vitabu vya kisheria kutoka 35 hadi vitano kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 2015, kwa Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma,(katikati). Kushoto ni Msajili  wa Mahakama ya Rufani Tanzania, John Kahyoza.


Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma, akisoma kitabu kimojawapo.
 
                                           (Picha na Magreth Kinabo )

 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni