Jumatano, 6 Septemba 2017

CHUKUENI HATUA ZA KULINDA IMANI YA WANANCHI - KAMATI YA BUNGE.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeitaka Tume ya Utumishi ya Mahakama kuendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wa Mahakama watakaobainika kukiuka maadili na kuvunja sheria ili kuendelea kukuza na kuimarisha imani ya wananchi kwao.

Kauli hiyo ya Kamati imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Najma Murtza Giga baada ya kumalizika kwa kikao kati ya kamati hiyo naTume ya Utumishi wa Mahakama na Uongozi wa Mahakama nchini ambao uliongozwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba Bw. Amon Mpanju na Mtendaji Mkuu wa Mahakama  ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga.
Katika kikao hicho kilichofanyika jana, mjini Dodoma Tume ya Utumishi wa Mahakama iliwasilisha kwa kamati hiyo ya Bunge taarifa yake ya utekelezaji kwa mwaka 2016/2017.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Mhe. Giga aliiombaTume na Mahakama kwa ujumla kuendelea kuimarisha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kufanyakazi na Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini kwani kufanya hivyo kutaimarisha imani ya wananchi kwa huduma zitolewazo na Mahakama nchini.
Awali akiwasilisha taarifa hiyo Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bibi Enzeil Mtei alisema katika  kusimamia maadili na nidhamu za watumishi wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017 tume hiyo ilijadili na kufanya maamuzi juu ya masuala 76 ya nidhamu kwa watumishi wa kada mbalimbali ambapo 72 walifukuzwa kazi na wengine wanne walirejeshwa kazini.
Akizungumzia changamoto katika kushughulikia suala la ukosefu wa mafunzo kwa kamati za maadili, wamefanya mazungumzo na wadau mbalimbali ili kuona uwezekano wa kushirikiana nao katika eneo hilo.

Pia amesema wanaendelea kuzungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya wenye mamlaka ya kuendesha Kamati za Maadili za Mahakimu iliwatenge fedha na kutoa elimu kwa umma juu ya uwepo wa kamati hizo.
Naibu  Katibu  Mkuu  Wizara  ya  Katiba  na  Sheria  Bw. Amon  Mpanju (katikati )akiwa na  Mtendaji  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ,  Bw. Kattanga (kulia) na  Bibi, Katarina  Revokati , ambaye Msajili Mkuu wa Mahakama (kushoto) wakisilikiza taarifa  kutoka  Tume yaUtumishi wa Mahakama iliyokuwa ikiwasilishwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma.

Baadhi  ya  wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao, ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza  Tume ya Utumishi wa Mahakama iliyokuwa ikiwasilishwa kwa kamati hiyo.


Baadhi  ya  wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao, ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza  taarifa  ya  Tume ya Utumishi wa Mahakama iliyokuwa ikiwasilishwa kwa kamati hiyo.
(Picha  na  habari  na  Sheiba Bullu)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni