Jaji
wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara, Mhe. Lameck Mlacha pichani akisalimiana na
moja ya Mtumishi wa Mahakama pindi alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Mingoyo iliyopo
mkoani Lindi, hii ni moja kati ya
Mahakama ambazo Mhe. Mlacha ametembelea kukagua shughuli za Mahakama.
Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara, Mhe. Lameck Mlacha akiwa na baadhi ya Watumishi wa Mahakama-Lindi iliyopo chini ya Kanda ya Mtwara pindi alipotembelea Mahakama ya Mwanzo Mingoyo iliyopo mkoani Lindi.
Mhe. Jaji Mlacha akisaini rejesta pindi alipowasili Mahakama ya Mwanzo Mingoyo.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Mingoyo.
Mhe. Jaji Mlacha akikagua kiwanja cha Mahakama-Lindi chenye ukubwa wa hekari 52. Mpango wa Mahakama ya Tanzania ni kujenga Mahakama Kuu katika mkoa huo ili kusogeza huduma za utoaji haki kwa wananchi wa mkoa huo ambao husafiri kwenda Mahakama Kuu-Mtwara kupata huduma ya Mahakama Kuu.
Mhe.Jaji akiongea na baadhi ya wananchi
waliokuwa Mahakamani hapo kupata huduma za Kimahakama.
Akibadilishana mawazo na baadhi ya Watumishi wa Mahakama-Lindi.
Akikagua nyumba za Mahakama zilizojengwa na Mhe. Membe, Mahakama ya Rondo Lindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni