|
Mwenyekiti wa Bodi
ya Uongozi wa Chuo cha Uongozi
wa Mahakama(IJA), Lushoto Jaji
Mstaafu, Mhe. John Mrosso( wa
kwanza kulia) akisikiliza
maelezo kuhusu hatua ya ujenzi wa cha Kituo
cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo ,
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
iliyopo jijini Dar es Salaam, kutoka
kwa Mtendaji
wa Mahakama hiyo, Bw. Gasto
Kanyairita(kushoto). (Kulia wa pili ) ni Mkuu wa
Chuo cha
Uongozi wa Mahakama (IJA) Mhe.
Jaji Dkt. Paul
Kihwelo. Hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo ni ukamilishaji wa uwekaji wa kuta ambao ulianza rasmi Agosti 29, 2017.
|
|
Baadhi ya mafundi wakiendelea
na ujenzi wa uwekaji kuta katika Kituo cha Mafunzo cha Mahakama
kilichopo, katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kituo
hicho kinachojengwa katika eneo la Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam
kitawaunganisha watumishi wa Mahakama na wadau katika mafunzo kwa njia ya video
(video conferencing).
|
Ujenzi huu, ni moja ya
Mpango Mkakati wa Mahakama ya
Tanzania wa Miaka Mitano 2015/2016 hadi
2019/2020 ikiwa ni hatua ya kuboresha utendaji kazi wa
watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
|
Ujenzi huu, ni moja ya
Mpango Mkakati wa Mahakama ya
Tanzania wa miaka mitano 2015/2016 hadi
2019/2020 ikiwa ni hatua ya kuboresha utendaji kazi wa
watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
|
|
(Picha na Mary Gwera)
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni