Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya Watanzania na kupambana na vitendo vya Rushwa.
Akizungumza wakati wa kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania leo Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amemtaka kiongozi huyo kufanya kazi kwa bidii licha ya changamoto zilizopo ndani ya Mhimili wa Mahakama kwa kuwa Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na Mhimili huo.
“Mungu amekuchagua, katumikie watu kwa kuongozwa na maslahi ya wananchi”, alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa tatizo la rushwa ni kubwa na liko katika kila chombo cha Serikali hivyo alimtaka kiongozi huyo kupambana nalo.
Rais alisema pamoja na kuwepo kwa Majaji wengi ambao ni watendaji wazuri, ameamua kumchagua Prof. Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuwa dhamira yake imemkubali kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kupambana na vitendo vya Rushwa.
Akielezea sababu ya kuchelewa kuteua Jaji Mkuu, Mhe. Rais alisema alijipa muda ili ateue mtu atakayekaa muda mrefu kwenye nafasi hiyo na siyo mtu aliyebakisha muda mchache kustaafu Utumishi wa Mahakama. Hata hivyo, Mhe. Rais alisema Ibara ya 118 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu kidogo cha 4 inampa Mamlaka ya kuteua Kaimu Jaji Mkuu kabla ya kumteua Jaji Mkuu.
Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema hakuna mgongano baina ya mihimili yote mitatu ya dola kwa kuwa yote inafanya kazi ya kuboresha maslahi ya wananchi wa Tanzania na kuwa katiba ya nchi inalazimisha ushirikiano baina ya mihimili yote.
Jaji Mkuu alisema, Mahakama imejiwekea utaratibu wa kuondoa uwezekano wa kutokea kwa migangano baina ya mihimili kwa kuzupa kipaumbele kesi zinazohusiana na kazi zinazofanywa na Serikali kama vile ujenzi wa reli au barabara, migogoro ya wakulima na kesi ,mbalimbali za uhujumu uchumi.
Aidha, Prof. Juma alimshukuru Rais kwa kumteua kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania na kuahidi kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati kwa kuwa hiyo ndiyo kazi moja kubwa ya Mahakama ya Tanzania.
Alisema Mahakama ya Tanzania inatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia nguzo tatu za Mpango Mkakati wake wa miaka mitano ambazo ni Utawala bora na usimamizi wa rasilimali, Upatikanaji wa Haki kwa wakati pamoja na urejeshaji wa imani ya wananchi kwa Mahakama.
Alizitaja baadhi ya changamoto ndani ya Mahakama alizokabiliana nazo akiwa Kaimu Jaji Mkuu na pia atakazokabiliana nazo kama Jaji Mkuu kuwa ni upungufu wa majengo ya Mahakama hasa Mahakama za Mwanzo nchini. Alisema Tanzania ina kata 4000 ambapo kati ya hizo, ni kata 976 pekee ndizo zenye Mahakama za Mwanzo.
Wakati huo huo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jaji Mkuu katika majukumu yake ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata haki kwa wakati.
Aidha, Waziri huyo wa Katiba na Sheria pia alimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua Prof. Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuwa ni mchapa kazi, mtii na muadilifu.
Prof. Juma aliapishwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Januari 18, 2017 na kuteuliwa rasmi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Septemba 10, 2017 ambapo leo Septemba 11, 2017 ameapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Prof. Juma anakuwa ni Jaji wa 8 tangu nchi ipate uhuru na Jaji wa 6 Mzalendo.
Majaji hao ni Raphs Windham (1961-1964), Telford Georges (1965-1970), Augustino Said- Jaji wa kwanza Mzalendo (1971-1977), Francis Lucas Nyalali (1977-2000), Barnabas Albert Samatta (2000-2007), Augustino Ramadhani (2007-2011), Mohamed Chande Othman (2011-2017) na Prof. Ibrahim Hamis Juma wa sasa.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema Septemba 11, hafla hiyo fupi ya
uapishwaji wa Mhe. Jaji Mkuu imefanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es
Salaam. Mhe. Jaji Mkuu amethibitishwa katika nafasi hiyo ya Ujaji Mkuu baada ya kutumikia nafasi ya Kaimu Jaji Mkuu kuanzia Januari 18, hadi Septemba 10 mwaka huu.
Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Wageni wengine waalikwa wakishuhudia kuapishwa kwa Mhe.Jaji Mkuu (hayupo pichani)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumwapisha Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania.
Mhe. Rais akimkabidhi hati ya Kiapo huku akimpongeza Mhe Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kumuapisha rasmi kushika nafasi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe akiongea neno mara baada ya kumuapisha Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Rais amemtaka Mhe. Jaji Mkuu kutetea haki za wanyonge na kupambana na rushwa ili kusukuma gurudumu la maendeleo. aliyeketi wa kwanza kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, wa pili kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai na wa kwanza kushoto ni Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi, Eng. John Kijazi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, akiongea jambo pindi alipopata nafasi ya kutoa neno mara baada ya kuapishwa kwake, Mhe. Prof. Juma amesisitiza juu ya upatikanaji wa haki kwa wakati kwa wananchi wa aina zote.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba M. Kabudi akiongea neno katika hafla ya kuapishwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Mhe. Waziri amemuhakikishia kumpa ushirikiano katika utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akiongea katika hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Ndugai amemhakikishia Mhe. Jaji Mkuu kumpa ushirikiano katika utendaji kazi.
Mihimili ya Dola: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania (kushoto) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai.(kulia)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mballimbali wa Serikali, wa tatu kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, wa pili kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, wa tatu kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Yustino Ndugai, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na wa kwanza kulia ni Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman.
Baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB).
Baadhi ya Viongozi wa Mahakama wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria katika hafla ya uapishwaji wa Mhe. Jaji Mkuu, waliosimama nyuma wa tatu kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa tatu kulia ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, wa kwanza kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi, Mhe. Phocus Bampikya, wa kwanza kushoto ni Msajili-Mahakama Kuu, Mhe. Ilvin Mugeta, katikati ni Mhe. Angelo Mapunda, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na wa pili kushoto ni Mhe. Georgina Mulebya, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma pamoja na familia yake wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, wa pili kulia ni Mke wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Bi. Marina P. Juma.
Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa Serikali.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni