Jumatatu, 6 Novemba 2017

MTENDAJI MPYA WA MAHAKAMA KANDA YA DODOMA AJITAMBULISHA


Mtendaji, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Bi. Maria Francis Itala (wa pili kulia) akiwa katika ziara ya utambulisho katika Mahakama za Wilaya zilizopo Mkoani Dodoma mara baada ya kuripoti katika kituo chake kipya cha kazi kufuatia uhamisho wake kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Pichani: Mtendaji wa Mahakama alipotembelea eneo la Mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kondoa akifanya mazungumzo na Wataalamu na Mafundi wa Kampuni ya Moladi akiwa katika ziara ya kikazi.
Muonekano wa jengo chakavu la Mahakama ya Mwanzo Bereko ambapo Bi.Itala alitembelea alipokuwa katika ziara yake, Aidha; Mtendaji huyo alikagua maendeleo ya Mradi wa umaliziaji wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo Bereko.
 Ukaguzi wa Majengo ya Mahakama- Mkoani Dodoma. 
(Picha na Stanslaus A. Makendi, Dodoma)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni