MAHAKAMA
TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa na taarifa inayosambazwa kwenye mitandao
ya kijamii kupitia bango la kitambaa lililoandikwa ujumbe kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli, ujumbe
huo ukimtuhumu Mhe.
Frederica Mgaya (Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu) kudhulumu haki ya kurithi kwenye Shauri la
Mirathi Namba. 81 la mwaka
2006. Ujumbe huo unamwomba. Mhe Rais kumwajibisha Jaji Mgaya.
Mahakama ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuwa taarifa hiyo si
ya kweli, na tunapenda kutoa ufafanuzi wa kuhusu suala linalolalamikiwa kama
ifuatavyo:
Kwamba,
Mhe. Jaji Mgaya hajawahi kusikiliza shauri la mirathi Na. 81/2006 na wala
Mahakama ya Ardhi ambayo Jaji huyo alikuwa akifanya kazi haina mamlaka ya
kusikiliza mashauri ya mirathi;
Kwamba,
Mhe. Jaji Mgaya amewahi kusikiliza shauri la Ardhi Na. 329/ 2015, hata hivyo
wanaotoa ujumbe huo hawakuwa sehemu ya shauri hilo.
Kwamba
baada ya uamuzi wa shauri Na. 329/2015 kutolewa, mlalamikaji aliandika
malalamiko yanayoonyesha kuwa aliona amenyimwa haki kwani alitamani awe sehemu
ya shauri hilo. Hatua za kisheria zilichukuliwa na Mahakama na kulifunguliwa
shauri la Mapitio (Revision) namba 6 la mwaka 2017 katika Mahakama ya Rufani ya
Tanzania.
Siyo kweli
kwamba Jaji ameiba jalada la Mahakama kwani jalada hilo limeitishwa Mahakama ya
Rufani kwa ajili ya mapitio baada kupokea malalamiko toka kwa mlalamikaji.
Shauri la
Mapitio (Revision) bado linaendelea katika Mahakama ya Rufani na anayelalamika
katika bango alifika Mahakamani mwezi Julai, 2017 shauri lilipopangwa kusikilizwa.
Aidha,
kutokana na suala hilo kuwa bado liko Mahakamani na linasubiri uamuzi wa
Mahakama, Mahakama ya Tanzania kwa sasa inazuiliwa kutoa maelezo ya kina juu ya masuala mengine
yaliyolalamikiwa.
Mahakama ya Tanzania inauhakikishia Umma kwamba itaendelea kutoa
huduma kwa misingi ya Katiba na sheria za nchi bila upendeleo huba wala chuki.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI
MAHAKAMA YA TANZANIA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni