Jumatano, 14 Machi 2018

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KIKAO KAZI CHA KUTATHMINI MPANGO MKAKATI PAMOJA NA MRADI WA MABORESHO YA HUDUMA ZA MAHAKAMA

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati (mwenye kikoi chekundu ) pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama wanawake wakifurahia zawadi za vikoi walivyopewa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (hayupo pichani) kwa niaba ya wanawake wote wa Mahakama wakati sherehe ya Siku ya wanawake Duniani, wakiwa katika kikao kazi cha kutathmini Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama kinachoendelea jijini Arusha.
 Baadhi ya waheshimiwa Mahakimu wanawake wakifurahia zawadi za vikoi mara baada ya kukabidhiwa. Wa pili kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara Mhe. Elizabeth Missana akifuatiwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama Mhe. Evodia Kyaruzi.
 Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanawake wakifurahia zawadi 
 
  Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanawake wakifurahia zawadi

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama ya Tanzania, Bibi Wanyenda Kutta akiwa ameshika zawadi za vikoi kwa ajili ya kuwakabidhi  (kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Kattanga) Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanawake wakati wa sherehe ya Siku ya wanawake Duniani, wakiwa katika kikao kazi cha kutathmini Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama kinachoendelea jijini Arusha.
 
 Watumishi wa Mahakama wakiwemo Watendaji, Manaibu Wasajili na wataalamu wengine mbalimbali wakiwa katika kazi za vikundi ikiwa ni hatua ya kutathmini Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama katika kikao kazi kinachoendelea jijini Arusha. 
 Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya akiwa pamoja na watumishi wengine wa Mahakama wakitathmini Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama katika kikao kazi kinachoendelea jijini Arusha. 
 Watumishi wa Mahakama wakiwemo Watendaji, Manaibu Wasajili na wataalamu wengine mbalimbali wakiwa katika kazi za vikundi ikiwa ni hatua ya kutathmini Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama katika kikao kazi kinachoendelea jijini Arusha. 
 
 Watumishi wa Mahakama wakiwemo Watendaji, Manaibu Wasajili na wataalamu wengine mbalimbali wakiwa katika kazi za vikundi ikiwa ni hatua ya kutathmini Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama katika kikao kazi kinachoendelea jijini Arusha. 
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Joachim Tiganga akiwasilisha mada ya kikundi katika kikao kazi cha kutathmini Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama katika kikao kazi kinachoendelea jijini Arusha. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni