Jumatano, 2 Mei 2018

MAHAKIMU NA MAWAKILI WATAKIWA KUZINGATIA MATAKWA YA KISHERIA KUENDESHA MASHAURI

Na Amina Ahmad, Tanga
Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania wamewaagiza Mahakimu na Mawakili wazingatie matakwa ya kisheria katika kufungua, kuendesha mashauri na kutoa maamuzi mbalimbali Mahakamani.
Maagizo hayo yametolewa na Wheshimiwa Majaji hao wakati wa mkutano wa kufunga kikao cha Mahakama ya Rufani (Post Session) uliofanyika hivi karibuni Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Tanga

Aidha, Mwenyekiti wa Jopo la kikao hicho, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk alieleza masuala mbalimbali ya kisheria ambayo ni bora Mahakimu na Mawakili kujifunza namna gani ya kukuyatekeleza ili kusiwepo tena na mashauri kurudishwa Mahakama za chini kwa ajili ya kurudiwa (retrial).

Aliwataka pia Mahakimu, Mawakili pamoja na wadau wote kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa misingi ya sheria katika kuendesha mashauri.
Wakati huo huo, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Elizabeth Mkwizu amesema asilimia 88 ya mashauri yamemalizika na mashauri matatu kuahirishwa kwa sababu mbalimbali katika kikao cha Mahakama ya Rufani kilichofanyika hivi karibuni kwenye Kanda hiyo.

Naye amesema Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga Mhe. Adrian Kilimi amesema baada ya kumalizika kwa kikao cha Mahakama ya Rufani hivi sasa masijala ndogo ya Rufaa mkoani Tanga haina mashauri ya mlundikano (Backlog).
Jumla ya Mahakimu 27, Mawakili wa Serikali 9, waendesha mashtaka Takukuru 4 na Mawakili wa kujitegemea 26 kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Tanga walishiriki kikao hicho.

  Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. Elizabeth Mkwizu (kulia), akifuatiwa na Naibu Msajili wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga Mhe. Adrian Kilimi na kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga Mhe. Crisencia Kisongo wakiwa kwenye Kikao.
  Mwakilishi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Naimani Shose akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa kufunga kikao cha Mahakama ya Rufani.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Mhe. Cornel Egbert Mujungu akichangia mada katika Mkutano huo.

  Mwenyekiti wa Majaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Mbarouk (wa pili kulia), akifuatiwa na Mhe. Sivangilwa Mwangesi na kushoto kwake ni Mhe. Jaji. Augustine Mwarija wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga Mhe. Amour Khamis pamoja na Naibu Wasajili mara baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.

  Wahe. Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu

  Wahe. Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mawakili wa serikali

  Wahe. Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mawakili wa Kujitegemea

     Wahe. Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau kutoka Jeshi la Magereza na Waendesha Mashtaka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni