Mwenyekiti wa
Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania ambaye pia ni Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Naibu Wasajili, Watendaji,
Mahakimu na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Mahakama kutenda haki kwa
watumishi walio chini yao kwani kimbilio la Mtumishi anapopata matatizo
ni kwa kiongozi wake katika sehemu yake ya kazi.
Akifungua Mkutano
wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania leo mjini Dodoma, Jaji Mkuu
amesema endapo viongozi hao watajifungia na kutojihusisha na matatizo ya
watumishi walio chini yao ni wazi kuwa morali ya utendaji kazi itashuka, tija
itakosekana na hivyo wananchi watapewa huduma zisizoridhisha hasa katika
kipindi hiki ambapo Mahakama ya Tanzania inaendelea na maboresho ya kisayansi
ya huduma zake.
“Kiongozi sehemu
ya kazi ni yule anayehamasisha na kuelimisha kwa kuonyesha njia mpya,
anasikiliza, anajifunza na anakubali kuwa mfanyakazi anaweza kumfungus macho,”
alisema Jaji Mkuu.
Aidha, Jaji Mkuu
pia amewataka Viongozi hao kuacha tabia ya ubwana bali watekeleze wajibu wao
kwa kuwaongoza watumishi walio chini yao kwa ustaarabu na uadilifu.
Alisema Mahakama
ya Tanzania imeamua kufanya kazi kisayansi na kwa malengo na misingi
inayokubalika kwa vitendo na kwa mujibu wa Sheria na itatekeleza hilo kwa
kuhakikisha kuwa inakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa
Maendeleo wa miaka mitano (2016/17-2020/21) kupitia Mpango Mkakati wa miaka
mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/16-2019/20) ambao unatekelezwa kwenye
maeneo matatu muhimu.
Aliyataja maeneo
hayo kuwa ni Utawala Bora, Uwajibikaji na Usimamizi wa Rasilima, Upatikanaji wa
Haki kwa wakati pamoja na Uimarishaji wa imani ya wananchi kwa Mahakama na
ushirikishwaji wa wadau kwenye shughuli za Mahakama.
Jaji Mkuu alisema
ili kutekeleza Mpango huo wa Maendeleo wa Taifa, Watumishi wa Mahakama hawana
budi kujiona kuwa wao ni sehemu ya mabadiliko na kwamba mabadiliko yaliyopo
sasa ndani ya Mahakama yanatokana na wao kutoa huduma bora kwa wananchi.
Alisema
imeshirikisha Watumishi wake katika hatua mbalimbali za kujenga Mpango Mkakati
na kutekeleza kwa vitendo. Kupitia baraza la katika utoaji wa huduma za
mahakama kuepuka migogoro isiyo ya lazima sehemu za kazi.
Mabaraza ya
Wafanyakazi sehemu za kazi yanaundwa kwa mujibu wa Sheria na Miongozo ambayo ni
Agizo la Rais namba 1 la mwaka 1970, Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya
mwaka 2002 pamoja na kanuni zake za mwaka 2003 na Sheria ya Majadiliano ya
pamoja katika Utumishi wa Umma Namba 19 ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake za
mwaka 2005.
Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akifungua Mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania jana mjini Dodoma.
|
Wafanyakazi
wa Mahakama ya Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa
Mahakama ya Tanzania jana mjini Dodoma.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni