Muonekano wa Banda la Mahakama ya Tanzania
lililopo katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini
Dar es Salaam, katika Maonesho haya Mahakama ya Tanzania imejipanga kutoa
huduma ya utoaji elimu juu ya taratibu mbalimbali za kimahakama, matumizi ya
tehama mahakamani, elimu kuhusu ufanyaji kazi wa mahakama inayotembea ‘mobile
court’.
Huduma nyingine zitakazotolewa ni pamoja na masuala ya mirathi, ardhi, kazi pamoja na kusikiliza na kutolea suluhu malalamiko ya wananchi watakaopata fursa ya kutembelea banda la mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni