Na
Lydia Churi
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwemo Mahakimu na Wasaidizi wa Kisheria wa Waheshimiwa Majaji wanahudhuria mafunzo ya siku tatu juu ya utoaji wa Taarifa za Maamuzi na Sheria kwa njia ya mtandao bure yatakayosaidia kuboresha utendaji kazi wao.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwemo Mahakimu na Wasaidizi wa Kisheria wa Waheshimiwa Majaji wanahudhuria mafunzo ya siku tatu juu ya utoaji wa Taarifa za Maamuzi na Sheria kwa njia ya mtandao bure yatakayosaidia kuboresha utendaji kazi wao.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa ufadhiliwa wa Chuo kikuu cha Cape Town cha Afrika ya Kusini kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la masuala ya sheria nchini Kenya, (Kenya Law -National Council for Law Reporting).
Aidha, mafunzo hayo yaliyoanza
jana katika ofisi za kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama
ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit-JDU) jijini Dar es salaam yanawakutanisha baadhi
ya Mahakimu pamoja na Wasaidizi wa Kisheria wa waheshimiwa Majaji ili kuwajengea
uwezo katika utendaji wa kazi zao.
Mafunzo hayo yalianza Juni
26 na yanatarajiwa kumalizika Juni 28, 2018.
Katika kutekeleza
Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16
hadi 2019/2020) pamoja na Mradi wa Maboresho ya huduma za Mahakama,
Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imekuwa ikitoa mafunzo
kwa watumishi wake wa ngazi mbalimbali ili kuboresha huduma kwa wananchi, kutoa
haki kwa wakati na kurejesha imani ya wananchi kwa Mhimili huo.
Baadhi ya Mahakimu na Wasaidizi wa Kisheria wa Majaji wakiwa kwenye Mafunzo juu ya Utoaji wa Taarifa za Maamuzi na Sheria kwa njia ya Mtandao bure yanayotolewa na Chuo kikuu cha Cape Town cha Afrika ya Kusini kwa kushirikiana Baraza la Taifa la masuala ya Sheria nchini Kenya, Kenya Law- National Council For Law Reporting) jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mahakimu na Wasaidizi wa Kisheria wa Majaji wakiwa kwenye Mafunzo juu ya Utoaji wa Taarifa za Maamuzi na Sheria kwa njia ya Mtandao bure wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva (katikati) akiwa na wawakilishi kutoka Kenya Law (National Council For Law Reporting), Njeri Githang'a (kulia) na Christian Ateka.
Mwakilishi kutoka Kenya Law (National Council For Law Reporting), Njeri Githang'a akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Mahakimu na Wasaidizi wa Kisheria wa Majaji wakiwa kwenye Mafunzo juu ya Utoaji wa Taarifa za Maamuzi na Sheria kwa njia ya Mtandao bure yanayotolewa na Chuo Kikuu cha Cape Town cha Afrika ya Kusini kwa kushirikiana na Kenya Law (National Council For Law Reporting) jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Mahakimu na Wasaidizi wa Kisheria wa Majaji wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mafunzo hayo.
(Picha na Lydia Churi-Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni