JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
YA TANZANIA
TANGAZO KWA UMMA.
MAHAKAMA
YA TANZANIA ITASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YAANI ‘SABASABA’, YATAKAYOANZA RASMI TAREHE 28.06.2018 HADI TAREHE 08.07.2018.
JE,
UMEDHULUMIWA NA KUPORWA HAKI YAKO?
JE, UNA
MATATIZO YANAYOKUNYIMA HAKI YAKO YA MIRATHI?
JE,
UNAHITAJI NAKALA YA HUKUMU YAKO NA HUJAIPATA?
JE,
UNATAKA KUFAHAMU NA KUELIMISHWA ZAIDI KUHUSU MAHAKAMA YA TANZANIA?
TEMBELEA
BANDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA
KATIKA
MAONESHO HAYA, MAHAKAMA YA TANZANIA INAKUSUDIA KUTOA HUDUMA MBALIMBALI KWA
WANANCHI, NA ITATOA ELIMU JUU YA
·
TARATIBU
MBALIMBALI ZA KIMAHAKAMA,
·
MATUMIZI
YA TEHAMA MAHAKAMANI,
·
UTHIBITISHAJI
NA UTIAJI SAHIHI WA NYARAKA MBALIMBALI
·
MASUALA
YA MIRATHI, ARDHI, KAZI, BIASHARA, MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI
·
PAMOJA NA
KUSIKILIZA NA KUTOLEA SULUHU MALALAMIKO YA WANANCHI WATAKAOPATA FURSA YA KUTEMBELEA
BANDA LA MAHAKAMA.
HUDUMA
HIZO ZITATOLEWA KWENYE BANDA LA MAHAKAMA, LINALOPATIKANA MKABALA NA BANDA LA
JKT LILILOPO KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO VYA MWALIMU NYERERE, BARABARA YA KILWA,
JIJINI DAR ES SALAAM.
EWE
MWANANCHI, KARIBU UPATE HUDUMA NA ELIMU YA SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO YATAKAYOCHANGIA
KATIKA KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.
NYOTE
MNAKARIBISHWA.
IMETOLEWA
NA;
KITENGO
CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
MAHAKAMA YA TANZANIA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni