Jumatatu, 25 Juni 2018

RAIS AMTEUA JAJI NDIKA KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA UONGOZI WA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA


                                         TAARIFA KWA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Dkt.Gerald Ndika kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Uteuzi huu umeanza tangu tarehe 17 Juni, 2018.

Mhe. Jaji Ndika anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. John Mrosso ambaye amemaliza muda wake baada ya kutumikia Baraza la Chuo hicho kwa muda wa takribani miaka sita.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO

MAHAKAMA YA TANZANIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni