Waheshimiwa Majaji walioapishwa
wakiwa katika picha ya pamoja, kushoto ni Mhe. Jaji Ferdinand Wambali, Jaji
Mteule wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi wake Mhe. Jaji Wambali alikuwa
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, katikati ni Mhe. Mwanaisha Kwariko,
Jaji Mteule wa Mahakama ya Rufani, kabla ya uteuzi wake, Jaji Kwariko alikuwa
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma na kulia ni Mhe. Jaji Dkt.
Eliezer Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kabla ya uteuzi
wake Mhe. Jaji Feleshi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya
Iringa.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Jaji
Ferdinand Wambali kuwa Jaji wa Mahakama yaRufani ya Tanzania, hafla hiyo fupi
ya kuapishwa Wahe. Majaji imefanyika Juni 04, 2018 katika Viwanja vya Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Mhe. Rais akimpa mkono
wa pongezi Mhe. Jaji Wambali mara baada ya kumuapisha rasmi kuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani.
Mhe. Rais akimuapisha
Mhe. Mwanaisha Kwariko kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Mhe. Rais akimpa mkono
wa pongezi Mhe. Mwanaisha Kwariko mara baada ya kumuapisha rasmi kuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani ya Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli (kushoto) akimuapisha, Mhe. Jaji
Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mhe. Rais akisaini hati
ya kiapo mara baada ya kumuapisha Mhe. Jaji Feleshi kuwa Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mkono wa pongezi mara
baada ya uapisho.
Aidha katika maneno yao
ya shukrani, Wahe. Majaji hao wameahidi kutekeleza majukumu yao ya kutumikia
wananchi kwa uadilifu, vilevile wamewataka Wadau wa Mahakama kushirikiana kwa
karibu na Mahakama ili kutekeleza jukumu kuu ya Utoaji haki nchini kwa wakati.
Waheshimiwa Majaji
wakila kiapo cha Maadili ya utendaji kazi mara baada ya kuapishwa kushika
nyadhifa zao mpya, kiapo hicho kiliongozwa na Kamishna wa Ofisi ya Sekretarieti
Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma, Mhe. Jaji Harold Nsekela, Jaji Mstaafu wa
Mahakama wa Rufani (T).
Baadhi ya Viongozi Wakuu
wa Serikali wakifurahia jambo katika hafla hiyo, wa kwanza kulia ni Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wa pili kulia
ni Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania, katikati ni Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kushoto ni Mhe. Prof.
Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria na wa kwanza kushoto ni Mhe.
Eng. John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi.
Picha ya baadhi ya
Majaji wa Mahakama ya Tanzania na Wageni wengine walioshiriki katika hafla hiyo
ya uapisho.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli (katikati) na Viongozi Wakuu wa
Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji walioapishwa, wawili
wakiwa Majaji wa Mahakaama ya Rufani na mmoja Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania.
Picha ya pamoja, Mhe.
Rais, Viongozi na baadhi ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa
katika picha ya pamoja na Majaji walioapishwa.
Meza Kuu ikiongozwa na
Mhe. Rais pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wateule.
Picha ya pamoja: Tume
ya Utumishi wa Mahakama na Majaji Wateule.
Mtendaji, Mahakama Kuu
ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (kulia), akikabidhi shada la maua kwa Mhe.
Jaji Ferdinand Wambali, Jaji wa Mahakama ya Rufani kama ishara ya pongezi kwa kuteuliwa
kwake, kabla ya uteuzi huu Mhe. Jaji
Wambali alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Mtendaji, Mahakama Kuu
ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (kulia), akikabidhi shada la maua kwa Mhe.
Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kama
pongezi kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo.
Picha ya pamoja, Wahe.
Majaji na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu.
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni