Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Mahakama ya Tanzania kuhusu masuala ya habari wakiwa kwenye Mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma.
Mafunzo ya Watumishi wa Mahakama ya Tanzania kuhusu masuala ya habari yanaendelea mjini Dodoma ambapo leo washiriki hao wamejifunza kuhusu upigaji wa picha za habari pamoja na namna ya kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii.
Mafunzo hayo yenye lengo
la kuwajengea uwezo Maafisa hao yanalenga kutekeleza nguzo ya tatu ya Mpango
Mkakati wa miaka mitano (2015/2016-2019/2010) wa Mahakama ya Tanzania yinayokusudia
kurejesha imani ya wananchi kwa Mahakama na kuwashirikisha wadau katika
shughuli za Mahakama.
Katika kutekeleza nguzo
ya tatu ya Mpango Mkakati huo, Mahakama ya Tanzania iliwateua baadhi ya Maafisa
wake wakiwemo Maafisa Utumishi, Maafisa Tawala, Maafisa Tehama na Wasaidizi wa
Kumbukumbu ili wasaidie kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya shughuli za
Mahakama hususan maboresho yanayoendelea ndani ya Mhimili huo wananchi wengi zaidi
wafahamu.
Aidha, mafunzo hayo ya
siku tano yanawashirikisha pia Maafisa Habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni
wadau wa Mahakama zikiwemo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Tume ya Kurekebisha Sheria na Wizara ya Sheria
na Katiba.
Mafunzo hayo ya siku
tano yameandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana na
Mahakama ya Tanzania chini ya udhamini wa Benki ya Dunia.
Mtaalamu wa Upigaji wa Picha za Habari Bw. Mwanzo Millinga akiwafundisha washiriki wa Mafunzo kuhusu kupiga picha za habari katika mafunzo yanayoendelea mjini Dodoma.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Mahakama ya Tanzania kuhusu masuala ya habari wakiwa katika Mafunzo kwa vitendo.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Mahakama ya Tanzania kuhusu masuala ya habari wakiwa katika Mafunzo kwa vitendo.
Mtaalamu akiwafundisha washiriki wa Mafunzo kuweka Picha za habari kwenye Blog.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Mahakama ya Tanzania kuhusu masuala ya habari wakiwa kwenye Mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni