Na Magreth Kinabo
Msajili Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati amewataka Mahakimu
walioajiriwa hivi karibuni kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Msajili huyo wakati akifungua mafunzo elekezi
kwa Mahakimu hao yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam.
Aidha Msajili
huyo aliwataka Mahakimu hao kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma
na kutojihusisha na ulevi, ugomvi na matumizi mabaya ya mitandao ya
kijamii kwa vitu visivyo kuwa vya kimaadili.
Kwa upande
wake Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Bw. Leonard Magacha
aliwataka mahakimu hao kuwa tayari kufanya kazi katika
maeneo waliyopangiwa hususan vijijini.
“ Nendeni
mkaripoti maeneo mliyopangiwa, mkafanye kazi bila
kuchagua maeneo,” alisema Magacha.
Mtendaji huyo
aliwataka Mahakimu hao kujitunza ili waweze kuepukana na maradhi.
Alisema
kwamba Mahakimu hao wanapaswa kufanya kazi kwa kujifunza kutoka kwa
watumishi wengine kwenye maeneo waliyopangiwa.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni