MAJAJI na Mahakimu
wameshauriwa kuzingatia sheria katika utoaji haki na wafuate miiko ya
kazi zao na kuhakikisha hawafanyi wanayoyataka wao.
Ushauri huo
ulitolewa mapema Julai 27, jijini Dar es Salaam na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya
Rufani, Mhe. Bernard Luanda katika hafla ya kuagwa kitaaluma yeye na Jaji
mstaafu wa mahakama hiyo, Sauda Mjasiri iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo
iliongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma na kuhudhuriwa
na watu mbalimbali wakiwemo Majaji wa mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama
Kuu, Majaji wastaafu wa mahakama ya Rufani.
"Kazi ya
kutoa haki ni ngumu, wanapokuja watu mahakamani kila mtu anavutia upande wake,
hivyo lazima utumie busara zako na sheria inasemaje,”alisema Jaji Mstaafu, Mhe.Luanda.
"Majaji na Mahakimu
wazingatie sheria, katika mahakama kila hatua ni sheria, lakini siyo sheria tu
imani ya wananchi kwa mahakama ni nguzo ya mahakama," alisema na kuongeza
wananchi ni muhimu kwa na imani na mahakama.
Alisema wananchi
wasipokuwa na imani na Mahakama ni hatari kwa kuwa wanaweza kujichukulia sheria mkononi.
Jaji mstaafu
Luanda alisema Majaji na Mahakimu wanapaswa kufanya kazi zao kwa kufuata miiko
na wasijaribu kufanya wanavyotaka wao na wasifanye vitu vya ajabu ajabu.
Mbali na hayo,
Jaji huyo Mstaafu ambaye ametumikia Mahakama kwa miaka 38, aliwaeleza Mahakimu
na majaji kuzingatia miiko 10 ya kazi zao ikiwemo ya kutojaribu kukwepa
majukumu yao katika kutoa uamuzi wa haki, kutojaribu kumtoa hatiani mtu kwa
kufahamu mwenendo wake mbaya, isipokuwa uwe umejiridhisha ametenda kosa
aliloshitakiwa nalo.
Pia, wasisite
kumwachia mtu ambaye ushahidi wake haujakamilika hata kama katika uelewa wako
inaonesha ametenda kosa, wasisite kumtoa hatiani mtu na kumwadhibu ipasavyo
kama ushahidi unaonesha ana hatia, bila kujali nafasi yake.
Jaji Mstaafu
Luanda amewaasa Majaji na Mahakimu kutokwenda nje ya ushahidi wa kesi na
kutotoa uamuzi kwa kufuata maoni ya ofisa wa mahakama, kutojadili kesi kabla
haijakufikia na usiruhusu kujadiliwa ikiwa ipo tayari kwenye mikono na vizuri
kujadili kesi ambayo imekuwa historia.
Jaji mstaafu
Luanda ambaye amestaafu akiwa ametumikia mahakama ya Rufani kwa miaka 10
aliwashukuru majaji wenzake, mahakimu, wasajili, manaibu wasajili na wafanyakazi
wengine kwa ushirikiano waliompatia katika utendaji wake wa kazi.
Naye Jaji mstaafu
Mjasiri alisema ametumikia mahakama ya Rufani kwa miaka 15 ambapo kabla ya hapo
amefanya kazi katika sehemu mbalimbali.
Jaji mstaafu
Mjasiri alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wadaawa ambao hawana uwakilishi
mahakamani kwenye mashauri mbalimbali katika Mahakama ya Rufani kuwa na
uwakilishi wa mawakili kwa kuwa hiyo ndiyo mahakama kubwa hapa nchini.
Alisema kwa kuwa
huyo ndiyo mahakama kubwa, wadaawa wa kesi wanaofika mahakamani
wanatakiwa wawakilishwe Ili kuhakikisha wanafuatilia kile kinachoendelea na
kipo sawa kwa ajili ya haki.
.
"Kwa kuwa mahakama ya Rufani ndiyo mahakama ya mwisho, ni muhimu wadaawa kuwakilishwa na mawakili anajua kuna hatua zinachukuliwa kufikia hatua hiyo, lakini zinahitajika za haraka.
.
"Kwa kuwa mahakama ya Rufani ndiyo mahakama ya mwisho, ni muhimu wadaawa kuwakilishwa na mawakili anajua kuna hatua zinachukuliwa kufikia hatua hiyo, lakini zinahitajika za haraka.
Alisema kwa kuwa
kuna wengine wakati wa usikilizwaji wa rufani wadaawa huamua kuachia kila kitu
kwenye mikono ya mahakama, kutokana na kutokuwa na uelewe wa kile kinachoendea.
"Hivyo Chama
cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinatakiwa kuangalia hilo kwa namna mawakili
wake watawawakilisha wadaawa ambao hawana uwakilishi," alisema.
Kwa upande wake,
Jaji Mkuu Profesa Juma alisema kwa kawaida baada ya majaji kustaafu wanaagana
kitaaluma ambapo Jaji Luanda ametumikia kwa miaka 37 huku Jaji Mjasiri akiwa
ametumikia sehemu mbalimbali na kutumikia mahakama kwa miaka 15.
Jaji Mkuu Profesa
Juma alisema hafla ya kuagwa kitaaluma, mbali ya kutoa ushauri inatoa nafasi
kwa majaji wengine wastaafu kukutana.
" Umri
wa kuishi Tanzania umeongezeka na majaji hawa wanaondoka wakiwa na nguvu zao na
wanaondoka wakiwa bado hazina," alisema Jaji Mkuu Profesa Juma.
Alisema
kinachotakiwa kuangaliwa ni namna gani wataendelea kuwatumia, hivyo vyuo vikuu
vinaweza kuwatumia kuwafundisha mawakili.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyeketi upande wa juu kulia) akiongoza hafla
ya kuwaaga kitaaluma Majaji wastaafu wawili wa Mahakama ya Rufani waliomaliza muda wao kwa
mujibu wa sheria, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe.
Benard Luanda, na aliyeketi kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Sauda Mjasiri.
Walioketi
mbele ya Wahe. Majaji kushoto ni Msajili, Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza
na kulia ni Mhe. Mpepo, Naibu Msajili Mahakama ya Rufani.
Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyeketi mbele wa kwanza kushoto)
pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Watendaji na
Watumishi wa Mahakama wakiwa katika sherehe ya kuwaaga Kitaaluma Waheshimiwa
Majaji wa Mahakama ya Rufani waliostaafu kwa mujibu wa sheria.
Mtendaji Mkuu-Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kulia) pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na baadhi ya Watendaji wengine wa Mahakama
wakiwa katika hafla hiyo.
Majaji wastaafu wa
Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, Mhe. Engela Kileo (aliyeketi mbele kulia)
na Mhe. Regina Rweyemamu pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika
sherehe hiyo.
Wageni waalikwa
wakifuatilia sherehe za kuwaaga kitaaluma Majaji wawili wastaafu wa Mahakama ya
Rufani Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) na Majaji wastaafu wa Mahakama ya Rufani,
Mhe. Benard Luanda (wa tatu kulia) na Mhe. Sauda Mjasiri wakiwa katika picha ya
pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati)
na Majaji wastaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda (wa tatu kulia) na
Mhe. Sauda Mjasiri wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania.
Picha ya pamoja na
Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na ZLS.
Mhe. Jaji Mkuu pamoja
na Majaji wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu wa Mhe. Benard Luanda,
Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Mhe. Jaji Mkuu pamoja
na Majaji wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu wa Mhe. Benard Luanda,
Jaji Msaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Mhe. Jaji Mkuu pamoja
na Majaji wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu wa Mhe. Sauda Mjasiri,
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Majaji Wastaafu wa
Mahakama ya Rufani wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kuagwa rasmi
kitaaluma baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria, kushoto ni Mhe. Benard Luanda
na kulia ni Mhe. Sauda Mjasiri, na katikati ni mke wa Mhe. Jaji Luanda.
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni