Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akizungumza jambo na baadhi ya
mahakimu wapya walioapishwa leo kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa
Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha na kulia ni Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu Masijala Kuu, Messeka Chaba.
Na Magreth
Kinabo
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe .Profesa Ibrahim Juma
amewataka mahakimu wapya wasiwe chanzo cha ucheleweshaji wa mashauri.
Aidha amewataka pia kuacha kulalamika bali pale linapotokea matatizo,
bali wawe chachu ya kuyatafutia ufumbuzi katika utendaji wao wa kazi wa
kutoa huduma za haki kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Mkuu huyo wakati
akiwaapisha Mahakimu wapya kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa
Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
“ Kiapo mlichoapa ni uzito muda wote mtakaofanya
kazi ya kuwatumikia
wananchi,
wananchi wanataka kutatuliwa kwa malalamiko yao kwa haraka,”alisema Jaji Mkuu.
Aliongeza kwamba
mfumo wa sasa sio wa kukaa na
kulalamika, kama kuna tatizo litafutiwe ufumbuzi na kuepuka kuwa chanzo
cha ulalamishi.
Alisema
mahakimu hao wanapaswa kuwa
weledi wanapotoa huduma za utoaji haki
ili waweze kutoa hukumu zinazoeleweka kwa kujibu wa sheria na kanuni. Hivyo wanapaswa kushirikiana na wadau wengine
wa mahakama ili kuahakikisha hukumu
zinatoka kwa haraka.
Alisisitiza mahakimu
hao kwamba kufanya kazi kwa kuepuka rushwa na kwa nidhamu.
Jaji Mkuu huyo
alifafanua kuwa changamoto za majengo chakavu na umbali , visikwamishe utendaji kazi
wao, hivyo mahakama iko katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano
ambao unalenga kutoa huduma za haki kwa wote na wakati, ikiwemo kuboresha miundombinu.
Aliwataka mahakimu hao kuielewa taasisi
inayofanyakazi na mpango mkakati huo.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni