Mtendaji wa Mahakama ya
Rufani, Bw. Solanus Nyimbi ametembelea banda la Mahakama ya Tanzania lililopo
katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Mtendaji huyo alitembelea
mapema Julai 06 na kujionea huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa ndani ya
Banda la Mahakama ya Tanzania.
Miongoni mwa huduma
zinazotolewa katika banda la Mahakama ni pamoja na Msaada wa Kisheria
unaotolewa na Chama cha Mawakili Tanganyika, utoaji elimu juu ya Menejimenti ya
Mashauri, Maboresho, Usimamizi wa Majengo, Mirathi, Mirathi na Malalamiko.
Ofisi nyingine
zinazopatikana katika banda hilo ni pamoja na Tume ya Utumishi wa Mahakama,
Tume ya Kurekebisha Sheria, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Chuo cha
Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
Aidha, Bw. Nyimbi
amewapongeza watoa huduma katika banda kwa kazi nzuri na kujipanga vyema katika
utoaji huduma hizo.
Mahakama ya Tanzania
inataraji kuhitimisha utoaji huduma tajwa Julai, 08, 2018 hivyo wananchi wote
wanahimizwa kuendelea kutembelea banda kupata huduma kabla ya kufungwa rasmi.
Mtendaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, Bw. Solanus Nyimbi akisaini kitabu cha Wageni pindi
alipowasili katika banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere almaarufu Sabasaba.
Mkurugenzi Msaidizi wa
Kumbukumbu za Utawala, Bw. Daniel Msangi (mwenye fulana nyekundu) akimueleza
Mtendaji juu ya huduma zinazotolewa katika banda la Mahakama.
Mtendaji akipata
maelezo kutoka sehemu ya Menejimenti ya Mashauri.
Mtendaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, Bw. Solanus Nyimbi akipata maelezo kutoka kwa Afisa kutoka Kitengo
cha Usimamizi wa Majengo-Mahakama, Mhandisi Coelestine Rutasindana pindi
alipotembelea banda la Mahakama mapema Julai 06.
Maafisa wa Mahakama wakisalimiana
na Mtendaji alipotembelea sehemu ya Malalamiko katika banda hilo.
Wananchi wakiendelea
kupata huduma ya msaada wa Sheria ndani ya banda la Mahakama.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni