Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mhe. Adelardus Kilangi (kushoto) akiuliza jambo pindi alipokuwa
akielezwa na Maafisa wa Mahakama juu ya upatikanaji wa nakala za hukumu kupitia
Tovuti ya Mahakama.
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mhe. Adelardus Kilangi (kulia) akiingia katika banda la Mahakama
pindi alipotembelea mapema Julai 06 kujionea huduma zinatolewa, kushoto ni Mhe.
Charles Magesa, Naibu Msajili- Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na
Uhujumu Uchumi.
Mhe. Charles Magesa,
Naibu Msajili- Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi akimuelezea
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Adelardus Kilangi (katikati) kuhusu huduma
zinazotolewa ndani ya banda la Mahakama.
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali akipata maelezo kutoka kwa Wanasheria waliopo sehemu ya TLS ambao
wanatoa msaada wa sheria kwa wananchi.
Mhe. Kilangi akisaini
kitabu cha wageni sehemu ya Malalamiko.
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali akisalimiana na Mwanasheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria ambao
pia wanapatikana ndani ya banda la Mahakama ya Tanzania.
Mhe. Kilangi akiuliza
jambo sehemu ya Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Watumishi wa Mahakama
wanaoshiriki katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba.
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni