Jumamosi, 7 Julai 2018

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, PROF. KABUDI ATEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA KATIKA MAONESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

 Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiwa ndani ya gari ya mfano inayotumika kama Mahakama inayotembea ‘mobile court’ pindi alipotembelea katika banda la Mahakama Julai 07, 2018.


Mhe. Waziri akisalimiana na Maafisa wa Mahakama waliopo sehemu ya Mirathi pindi alipotembelea banda la Mahakama lililopo Sabasaba.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akijadili jambo na Mkutubi sehemu ya Maktaba iliyopo katika banda la Mahakama.

 Mhe. Waziri akisalimiana na Maafisa wa Mahakama wanaopokea na kushughulikia Malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi wanaotembelea banda la Mahakama.

 Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano (kulia) akimueleza Mhe. Waziri jinsi kitengo hicho kinavyofanya kazi.


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (mwenye koti la brown) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Watumishi wa Mahakama wanaoshiriki kutoa elimu kwa umma katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni