Jumanne, 3 Julai 2018

MTENDAJI MKUU MAHAKAMA YA TANZANIA ATEMBELEA MAONESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA


Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akisaini kitabu cha wageni pindi alipowasili katika banda la Mahakama ya Tanzania lililopo kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).


Mtendaji Mkuu akiwa sehemu yaKurugenzi ya Menejimenti ya Mashauri iliyopo katika banda la Mahakama, kushoto ni baadhi ya Watumishi wa Idara hiyo wakishiriki katika kutoa huduma kwa wananchi kipindi hiki cha Maonesho ya Sabasaba.

 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania akifafanua kitu kwa mteja aliyetembelea sehemu ya Kitengo cha Usimamizi wa Majengo iliyopo ndani ya banda la Mahakama.

 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akipata huduma kutoka sehemu ya Idara ya Malalamiko ambayo pia ipo ndani ya banda la Mahakama.

 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga akisaini kitabu cha wageni pindi alipowatembelea Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) ambao pia wamo katika banda la Mahakama.


Mtendaji Mkuu akijadili jambo na Wanasheria wanaotoa huduma ya Msaada wa Sheria, Chama cha Wanasheria Tanganyika ni moja ya Wadau waliopo katika banda la Mahakama katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa.


Mtendaji Mkuu akijadili jambo na Maafisa Habari wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano-Mahakama alipotembelea sehemu hiyo.
Aidha Mtendaji Mkuu amewataka Washiriki wote wanaoiwakilisha Mahakama katika Maonesho hayo kuwahudumia wanananchi kwa ufasaha.
(Picha na Mary Gwera)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni