Jumanne, 3 Julai 2018

MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA YA TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akiwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha katika ofisi za Tantrade zilizopo kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati (katikati) akiwasili kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akishuka kwenye gari maalum linalotumika kama Mahakama inayotembea (Mobile Court)lililopo kwenye viwanja vya Maonesho -Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akimsikiliza Mtumishi wa Mahakama, Moses Ndelwa akielezea namna Mahakama inayotembea itakavyofanya kazi. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi (Kumbukumbu za Utawala), Bwn. Daniel Msangi.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama ya Tanzania Bibi Wanyenda Kutta alipowasili kwenye banda la Mahakama ya Tanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama ya Tanzania Bibi Wanyenda Kutta akimuelezea jambo Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati.
 Afisa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania, Bibi. Bernadetha Barnabas akimuelezea Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati namna kitengo cha TEHAMA kinavyorahisisha utoaji wa Haki Mahakamani.
 Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Coelestine Rutasindana akimuelezea jambo Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akielezea jambo.
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akizungumza na Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Barbro-Johansson, Jackline Kimbe ambaye alitembelea banda la Maonesho la Mahakama. Jackline alielezea kiu yake ya kutaka kuwa Jaji katika siku za mbeleni.   
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akizwa katika picha ya pamoja na Mwanafunzi wa Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari ya Barbro-Johansson, Jackline Kimbe ambaye alitembelea banda la Maonesho la Mahakama. Jackline alielezea kiu yake ya kutaka kuwa Jaji katika
siku za mbeleni.   
Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bibi. Mary Gwera akimuelezea Msajili  Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati namna kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania kinavyofanya kazi zake hususan utekelezaji wa nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama (2015/16-2019/2020) inayohusu urejeshaji wa imani ya Wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau.

Maoni 1 :

  1. niwazo zuri kwa kueka maonesho hayo kila mwaka kwani inawapa hamasa wananchi kwa ujumla kujua kazi ya mahama na jinsi inavyojali haki za raia

    JibuFuta